Show simple item record

dc.contributor.authorKing`ei, Geofrey K
dc.date.accessioned2021-10-19T06:56:08Z
dc.date.available2021-10-19T06:56:08Z
dc.date.issued1992
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155622
dc.description.abstractTasnifu hii imeshughulika na kuhakiki moja wapo ya fani mashuhuri za fasihi, simulizi yaani methali. jambo moja muhimu ambalo tungelitaja hapa ni kwamba ingawaje tasnifu hii imetolewa kwa mahitaji ya shahada Y' Kiswahili, data ili~oehambuliwa humu ni kutoka katika lugha ya Kikambao Uchaguzi huu tuliufikia kwa kuhisi na kutambua umihimu llnaostahili kupewa fasihi katika lugha zetu nyingine za ~ Kiafrika katika vyuo na mashule yetu. Jambo kama hili linaambatana na juhudi zinazofanywa za kukuza na kustawisha I taanima zote zenye kukita katika misingi ya maish~ ya jamii za Kiafrika katika mataifa yetu maehangao Somo la tasnifu hii ni 'uhakiki wa 'Nthimo' (methali) za Kikamba' 0 Tumezihakiki methali hizi kwa kufuatisha misingi ya methali za Kiswahilio Hatukufanya hivyo kwa kutaka tu kulinganisha methali katika lugha za jamii hizi mbili bali kwa kuwa kwa kufanya hivyo tumetoa mianga zaidi kuonyesha kuwa methali ni ehombo maalumu eha mawasiliano katika jamii yoyote na pia jamii mbili zinazotofautiana kwa mengi huweza kuwa na mawazo sawa kuhusu mazingira yao na kadhalikao Mafunzo ya somo la fasihi simulizi ni mapya sana na hasa mashuleni ambapo somo hili litatahiniwa kwa mara ya kwanza mwaka huu. Masomo haya yamekuwa yakifunzwa katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwa miaka mingi lakini katika Kiingereza pekee" Hakuna kazi zozote tulizoweza kupata katika Kiswahili zilizotayarisha kwa shahada yoyote katika uwanja huu. ~unatumainia kuwa tasnifu hii itawachochea na kuwapa wengine shauku na hamu ya kutalii vipengelele kadhaa vya fasihi sirnulizina kuyasimulia yote katika Kiswahili na hivyo kuikwasisha na kuijenga fasihi ndilo lengo letu kuu katika kazi hii. Kama tulivyoeleza mwishoni mwa tasnifu, haiwezekani kuitalii fani yoyote ya fasihi kwa undani unaostahiki katika kazi ya upeo huu" Licha ya tatizo la wakati uliopo kuna vikwazo vingine vingi vinavyomkabili mkusanyaji na mchambuzi wa fasihi simulizi. Kunayo matatizo ya kuikusanya na kuipanga data sawa sawa na pia si jambo rahisi kupata maongozi thabiti ya kinadharia na Ki-isimu yenye msaada katika kazi kama hii. Katika tasnifu hii, tumechambua methali za Kikamba zisizozidi mia na ishirini ingawa tulikusanya zaidi ya methali mia tatu. Tulibidika kuchagua chache tu zilizotutimizia muradi wetu na vile vile kuziacha nyingine kwa sababu ya upeo wa kazi yetu" Mambo tuliyoshughulikia sana ni maumbile na matumizi ya 'nthimo' katika maisha ya jamii ya k{la siku" Hatukuweza ~uingilia sana nadharia za maana ya methali na jinsi inavyotofautiana nafani nyinginezo ama jinsi zinavyobunika na kadhalika kwa sababu tulizotaja hapo juu" Tasnifu hii ina sura nne kuu na moja fupi ya tano. Katika Sura ya Kwanza tunaeleza kwa muhtasari yote yanayonuiwa kutendwa katika tasnifu nzimao Tumeeleza lengo na madhumuni ya tasnifu, somo la tasnifu, nadharia zinazo tuongoza, maoni mbali mbali yaliyotolewa kuhusu somo hili na uwanja wa fasihi simulizi kwa ghafla, njia za utafiti na uhakiki zizizotumiwa na kadhalika. Mambo muhimu katika Sura ya Pili ni kuhusu maisha na utamaduni wa jamii ya Wakambao Tunaanza kwa kutoa maelezo mafupi juu ya historia ya Wakamba kabla ya kusimulia kwa ufupi mila zao tofauti ka~a vile kuzaliwa mtoto, ndoa, tohara, mazishi na kadhalika. Mazingira ya kijiografia wanamoishi na jinsi fani ya methali inavyofafanua mazingira na ada zao pia yamegusiwa~ Uaelezo haya yote kwa maoni yetu ni muhimu kwa vile methali ni sehemu ya utamaduni wa watu na kwa hivyo sharti iangaliwe vivyo Katika Sura ya Tatu, tumejaribu kujadili juu ya matatizo ya kuainisha inthimoi kama fani ya fasihi simulizi na pia tumetazama maumbile ya Kifasihi na Ki-isimu ya fani hii na kuzitolea maelezo mafupi kila moja wapo wa sifa tunazogusia. Nadharia ya 'maana' katika methali imejadiliwa tena kwa ufupi katika Sura ya Nne ambapo maoni ya wataalamu kadhaa wa lugha na fasihi yametajwaoVile vile katika Sura hii tumejadili kazi inazotimiza methali kama chombo eha mawasiliano. Mifano ya matumizi na kazi hizi kufuatana na nadharia ya iutunzi' (Literary Discourse Theory) ya Pratt (1974), yametolewao Mwisho tumejaribu kuonyesha rnatumiziya 'nthimo' tofauti kwa kutahadhanisha. Misemo humu imo katika Kikamba na pia tafsiri yake ya juu juu katika Kiswahili inaf atiwa na tafsiri ya unclani na mifano ya maelezo ya matumizi kama hayou Katika Sura ya Tano (Kiishilio) tunaeleza tena kiini eha kazi hii kwa jumla, misimamo tuliyofikia na rnatatizo tuliyopata kutokana na uehunguzi wetu wa 'nthlmo' na pia kutoa maoni na mapendekezo yetti kuhusu somo la tasnifu hii na jinsi utafiti zaidi ungeweza kuwa wa manufaa makubwa zaidioen_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleUhakiki Wa Nthimo (Methali) Za Kikamba: (Kwa Kufuatisha Misingi Ya Methali Za Kiswahili).en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States