Uhakiki Wa Nthimo (Methali) Za Kikamba: (Kwa Kufuatisha Misingi Ya Methali Za Kiswahili).
View/ Open
Date
1992Author
King`ei, Geofrey K
Type
ThesisLanguage
enMetadata
Show full item recordAbstract
Tasnifu hii imeshughulika na kuhakiki moja wapo ya fani
mashuhuri za fasihi, simulizi yaani methali. jambo moja
muhimu ambalo tungelitaja hapa ni kwamba ingawaje tasnifu
hii imetolewa kwa mahitaji ya shahada Y' Kiswahili, data
ili~oehambuliwa humu ni kutoka katika lugha ya Kikambao
Uchaguzi huu tuliufikia kwa kuhisi na kutambua umihimu
llnaostahili kupewa fasihi katika lugha zetu nyingine za
~
Kiafrika katika vyuo na mashule yetu. Jambo kama hili
linaambatana na juhudi zinazofanywa za kukuza na kustawisha
I
taanima zote zenye kukita katika misingi ya maish~ ya jamii
za Kiafrika katika mataifa yetu maehangao
Somo la tasnifu hii ni 'uhakiki wa 'Nthimo' (methali)
za Kikamba' 0 Tumezihakiki methali hizi kwa kufuatisha
misingi ya methali za Kiswahilio Hatukufanya hivyo kwa
kutaka tu kulinganisha methali katika lugha za jamii hizi
mbili bali kwa kuwa kwa kufanya hivyo tumetoa mianga zaidi
kuonyesha kuwa methali ni ehombo maalumu eha mawasiliano
katika jamii yoyote na pia jamii mbili zinazotofautiana
kwa mengi huweza kuwa na mawazo sawa kuhusu mazingira
yao na kadhalikao
Mafunzo ya somo la fasihi simulizi ni mapya sana na
hasa mashuleni ambapo somo hili litatahiniwa kwa mara ya
kwanza mwaka huu. Masomo haya yamekuwa yakifunzwa katika
Chuo Kikuu cha Nairobi kwa miaka mingi lakini katika
Kiingereza pekee" Hakuna kazi zozote tulizoweza kupata katika
Kiswahili zilizotayarisha kwa shahada yoyote katika uwanja huu.
~unatumainia kuwa tasnifu hii itawachochea na kuwapa wengine
shauku na hamu ya kutalii vipengelele kadhaa vya fasihi
sirnulizina kuyasimulia yote katika Kiswahili na hivyo
kuikwasisha na kuijenga fasihi ndilo lengo letu kuu katika
kazi hii.
Kama tulivyoeleza mwishoni mwa tasnifu, haiwezekani
kuitalii fani yoyote ya fasihi kwa undani unaostahiki katika
kazi ya upeo huu" Licha ya tatizo la wakati uliopo kuna
vikwazo vingine vingi vinavyomkabili mkusanyaji na mchambuzi
wa fasihi simulizi. Kunayo matatizo ya kuikusanya na kuipanga
data sawa sawa na pia si jambo rahisi kupata maongozi thabiti ya
kinadharia na Ki-isimu yenye msaada katika kazi kama hii.
Katika tasnifu hii, tumechambua methali za Kikamba zisizozidi mia
na ishirini ingawa tulikusanya zaidi ya methali mia tatu.
Tulibidika kuchagua chache tu zilizotutimizia muradi wetu na
vile vile kuziacha nyingine kwa sababu ya upeo wa kazi yetu"
Mambo tuliyoshughulikia sana ni maumbile na matumizi ya 'nthimo'
katika maisha ya jamii ya k{la siku" Hatukuweza ~uingilia sana
nadharia za maana ya methali na jinsi inavyotofautiana nafani
nyinginezo ama jinsi zinavyobunika na kadhalika kwa sababu
tulizotaja hapo juu"
Tasnifu hii ina sura nne kuu na moja fupi ya tano. Katika
Sura ya Kwanza tunaeleza kwa muhtasari yote yanayonuiwa
kutendwa katika tasnifu nzimao Tumeeleza lengo na
madhumuni ya tasnifu, somo la tasnifu, nadharia zinazo
tuongoza, maoni mbali mbali yaliyotolewa kuhusu somo hili
na uwanja wa fasihi simulizi kwa ghafla, njia za utafiti
na uhakiki zizizotumiwa na kadhalika.
Mambo muhimu katika Sura ya Pili ni kuhusu maisha
na utamaduni wa jamii ya Wakambao Tunaanza kwa kutoa
maelezo mafupi juu ya historia ya Wakamba kabla ya
kusimulia kwa ufupi mila zao tofauti ka~a vile kuzaliwa
mtoto, ndoa, tohara, mazishi na kadhalika. Mazingira ya
kijiografia wanamoishi na jinsi fani ya methali inavyofafanua
mazingira na ada zao pia yamegusiwa~ Uaelezo haya
yote kwa maoni yetu ni muhimu kwa vile methali ni sehemu
ya utamaduni wa watu na kwa hivyo sharti iangaliwe vivyo
Katika Sura ya Tatu, tumejaribu kujadili juu ya
matatizo ya kuainisha inthimoi kama fani ya fasihi simulizi
na pia tumetazama maumbile ya Kifasihi na Ki-isimu ya fani
hii na kuzitolea maelezo mafupi kila moja wapo wa sifa
tunazogusia. Nadharia ya 'maana' katika methali imejadiliwa
tena kwa ufupi katika Sura ya Nne ambapo maoni ya wataalamu
kadhaa wa lugha na fasihi yametajwaoVile vile katika
Sura hii tumejadili kazi inazotimiza methali kama chombo
eha mawasiliano. Mifano ya matumizi na kazi hizi kufuatana
na nadharia ya iutunzi' (Literary Discourse Theory) ya
Pratt (1974), yametolewao Mwisho tumejaribu kuonyesha
rnatumiziya 'nthimo' tofauti kwa kutahadhanisha. Misemo
humu imo katika Kikamba na pia tafsiri yake ya juu juu
katika Kiswahili inaf atiwa na tafsiri ya unclani na mifano
ya maelezo ya matumizi kama hayou
Katika Sura ya Tano (Kiishilio) tunaeleza tena
kiini eha kazi hii kwa jumla, misimamo tuliyofikia na
rnatatizo tuliyopata kutokana na uehunguzi wetu wa 'nthlmo'
na pia kutoa maoni na mapendekezo yetti kuhusu somo la
tasnifu hii na jinsi utafiti zaidi ungeweza kuwa wa
manufaa makubwa zaidio
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: