Maudhui Ya Siasa Na Athari Zake Katika Jamii: Mifano Kutoka Diwani Ya Kaza Macho
Abstract
Kwenye tasnifu hii, tumehakiki maudhui ya siasa na athari zake katika jamii. Diwani ya Kaza
Macho imerejelewa. Utafiti wetu ulilenga kutekeleza madhumuni matatu yafuatayo:
Kuchanganua namna maudhui ya kisiasa yanavyojitokeza katika diwani hiyo. Pili, kubainisha
athari za siasa kwa jamii. Na mwisho, kuchanganua mbinu za kisanaa ambazo zilitumiwa na
K.W. Wamitila kuendeleza maudhui ya siasa katika diwani hiyo. Nadharia ya uyakinifu wa
kijamii imetumika hapa. Mihimili ya nadharia hii ifuatayo ilitufaa sana: Wahusika
wameonyeshwa kwa njia ya kiuyakinifu, nadharia hii imesawiri matukio ya kihistoria na
wahusika wake kutekeleza matendo yao kitabaka. Utafiti wetu ulikuwa wa maktabani. Tulisoma
diwani Kaza Macho kwa kina na kunukuu katika shajara sehemu muhimu ambazo zinalenga
malengo yetu. Tulisoma magezeti mbalimbali, tasnifu za wasomi tofauti tofauti, vitabu vya ziada
pamoja na kupekua mtandao ili kupata data. Tulichanganua data hiyo kwa kuzingatia madhumni
ya utafiti wetu. Uchanganuzi wa data ulifanyika kwa kutumia njia ya uchambuzi wa kimaelezo
na ufafanuzi.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Arts [614]
The following license files are associated with this item: