Show simple item record

dc.contributor.authorMwanarusi, Lung'anzi
dc.date.accessioned2023-03-29T12:55:38Z
dc.date.available2023-03-29T12:55:38Z
dc.date.issued2022
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/163414
dc.description.abstractNyimbo ni mojawapo wa vipera vya fasihi simulizi. Nyimbo huweza kutofautiana au kulingana katika jamii moja hadi nyingine kutegemea mazingira ya jamii maalum. Utafiti huu ulishughulikia uchambuzi linganishi wa maudhui ya nyimbo za hodiya za jamii ya Wadigo wa Msambweni na Waswahili wa Jomvu Kuu. Utafiti huu uliongozwa na msingi wa nadharia ya uhalisia ambayo inahusu ulinganishi wa mambo kama yanavyotokea katika mazingira anayoishi binadamu. Tuliongozwa na madhumuni manne ambayo ni: kwanza, kuonyesha iwapo kuna usawa katika maudhui ya nyimbo za hodiya za Waswahili wa Jomvu Kuu na Wadigo wa Msambweni, pili, kuonyesha tofauti za kimaudhui zilizopo kati ya nyimbo za hodiya za Waswahili wa Jomvu Kuu na Wadigo wa Msambweni, tatu, kubainisha namna dini ya kiislamu inavyojitokeza katika nyimbo za hodiya za Waswahili wa Jomvu Kuu na Wadigo wa Msambweni na nne, kuchunguza ushirikiano na ujirani kati ya jamii hizi mbili, yaani jamii ya Waswahili wa Jomvu Kuu na Wadigo wa Msambweni unavyoathiri nyimbo zao za kazi. Kulingana na data ya utafiti wetu tuligundua ya kwamba yapo maudhui yanayofanana katika nyimbo za hodiya za jamii ya Wadigo wa Msambweni na jamii ya Waswahili wa Jomvu Kuu na ambayo ni: ushirikiano, umasikini, busara, biashara na bidii na kukashifu uvivu. Vile vile, tulibaini kuwa yapo maudhui machache tu yanayotofautiana katika nyimbo zao za kazi kukiwemo maudhui ya heshima na stara kwa Wadigo wa Msambweni na kwa upande wa Waswahili wa Jomvu Kuu tuliona maudhui ya uvumilivu, ulafi na uroho. Utafiti huu ni wa nyanjani na hivyo tulikusanya data kwa kwenda kwa watafitiwa wetu ambapo tulishirikiana nao katika kufanya kazi na pia tulitumia kamera kurekodi video ya nyimbo walizokuwa wakiziimba wakati wa kazi. Hatimaye, tulichanganua data iliyokuwa imepatikana kwa lugha ya nathari kwa kuzinakili nyimbo hizo kisha kuzitolea maelezo ya kiuchambuzi kulingana na madhumuni ya utafiti huu.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectUchambuzi Linganishi Wa Maudhui Katika Nyimbo Za Hodiya Za Wadigo Wa Msambweni Na Waswahili Wa Jomvu Kuuen_US
dc.titleUchambuzi Linganishi Wa Maudhui Katika Nyimbo Za Hodiya Za Wadigo Wa Msambweni Na Waswahili Wa Jomvu Kuuen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States