Uchambuzi Linganishi Wa Maudhui Katika Nyimbo Za Hodiya Za Wadigo Wa Msambweni Na Waswahili Wa Jomvu Kuu
View/ Open
Date
2022Author
Mwanarusi, Lung'anzi
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Nyimbo ni mojawapo wa vipera vya fasihi simulizi. Nyimbo huweza kutofautiana au kulingana katika jamii moja hadi nyingine kutegemea mazingira ya jamii maalum. Utafiti huu ulishughulikia uchambuzi linganishi wa maudhui ya nyimbo za hodiya za jamii ya Wadigo wa Msambweni na Waswahili wa Jomvu Kuu. Utafiti huu uliongozwa na msingi wa nadharia ya uhalisia ambayo inahusu ulinganishi wa mambo kama yanavyotokea katika mazingira anayoishi binadamu. Tuliongozwa na madhumuni manne ambayo ni: kwanza, kuonyesha iwapo kuna usawa katika maudhui ya nyimbo za hodiya za Waswahili wa Jomvu Kuu na Wadigo wa Msambweni, pili, kuonyesha tofauti za kimaudhui zilizopo kati ya nyimbo za hodiya za Waswahili wa Jomvu Kuu na Wadigo wa Msambweni, tatu, kubainisha namna dini ya kiislamu inavyojitokeza katika nyimbo za hodiya za Waswahili wa Jomvu Kuu na Wadigo wa Msambweni na nne, kuchunguza ushirikiano na ujirani kati ya jamii hizi mbili, yaani jamii ya Waswahili wa Jomvu Kuu na Wadigo wa Msambweni unavyoathiri nyimbo zao za kazi. Kulingana na data ya utafiti wetu tuligundua ya kwamba yapo maudhui yanayofanana katika nyimbo za hodiya za jamii ya Wadigo wa Msambweni na jamii ya Waswahili wa Jomvu Kuu na ambayo ni: ushirikiano, umasikini, busara, biashara na bidii na kukashifu uvivu. Vile vile, tulibaini kuwa yapo maudhui machache tu yanayotofautiana katika nyimbo zao za kazi kukiwemo maudhui ya heshima na stara kwa Wadigo wa Msambweni na kwa upande wa Waswahili wa Jomvu Kuu tuliona maudhui ya uvumilivu, ulafi na uroho. Utafiti huu ni wa nyanjani na hivyo tulikusanya data kwa kwenda kwa watafitiwa wetu ambapo tulishirikiana nao katika kufanya kazi na pia tulitumia kamera kurekodi video ya nyimbo walizokuwa wakiziimba wakati wa kazi. Hatimaye, tulichanganua data iliyokuwa imepatikana kwa lugha ya nathari kwa kuzinakili nyimbo hizo kisha kuzitolea maelezo ya kiuchambuzi kulingana na madhumuni ya utafiti huu.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Arts [607]
The following license files are associated with this item: