Bonde la wakati katika riwaya za Kezilahabi
Abstract
Tasnifu hii ni uhakiki wa riwaya nne za Kezi1ahabi
yaani Rosa Mistika (1971), Kichwamaji (1974), Dunia Uwanja
wa Fujo (1975) na Gamba la Nyoka (1979), ukidhamiria
kuchunguza jinsi ambavyo suala la bonde la wakati limemulikwa.
Lengo kuu la tasnifu hii ni kuonyesha uzito uliopewa dhana
ya bonde la wakati katika kuelezea mahusiano ya kijamii.
Imegawanyika katika sura sita. Katika sura ya kwanza
kuna mada ya tasnifu, somo la utafiti, madhumuni ya utafiti,
upeo wa tasnifu, yaliyofanywa kuhusu somo hili, msingi wa
nadharia, haipothesia na mwisho methodolojia.
Sura ya pili inamulika utamaduni wa kijadi na uie wa kigeni.
Nafasi ya dini pia imeshughulikiwa hapa.
Sura ya tatu inahusu mfumo wa elimu wa kimagharibi na
jinsi inavyoathiri mtazamo wa kizazi kipya.
Sura ya nne inaziangalia athari za kiuchumi-jamii
kwenye jamii.
Sura ya tano inahusu nafasi. ya siasa katika kuathiri
uhusiano wa wanajamii.
Sura ya sita ni hitimisho ambayo ni muhtasari wa yote
yaliyojadiliwa. Katika sura hii pia kuna sehemu inayoangalia
falsafa ya mwandishi na hatimaye sehemu inayozizungumzia
riwaya za hivi karibuni za Kezilahabi yaani Nagona (1990)
na Mzingile (1991)
Citation
Tasnifu hii imetolewa ill kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahadaPublisher
Department of Arts