Show simple item record

dc.contributor.authorOsiemo, Donald O
dc.date.accessioned2013-05-02T11:15:43Z
dc.date.available2013-05-02T11:15:43Z
dc.date.issued1997
dc.identifier.citationMasters of education thesis,University of Nairobi (1997)en
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/18351
dc.description.abstractTasnifu hii imeshughulikia fani katika ushairi wa Hassan Mwalimu Mbega. Tumehakiki diwani zake mbili ambazo ni Upisho wa umalenga (1975) na Dafina ya Umalenga (1984) kwa kutumia nadharia ya urasimu. Kuna sura tano katika tasnifu. Sura ya kwanza ni ya utangulizi ama pendekezo la utafiti. Ni sura inayohusu somo la utafiti, madhumuni ya utafiti, upeo na mipaka ya utafiti, sababu za kulichagua somo, haipothesia, yaliyoandikwa kuhusu somo, msingi wa nadharia na njia za utafiti. Sura ya pili ambayo ni ya misingi ya uhakiki inahusu uamili wa lugha ya kishairi katika sanaa, sifa zake, na namna inavyoshirikiana au kutumiwa katika ploti. Tumeangalia umuhimu wa kila mojawapo ya vipengele hivyo na mchango wao katika fani kwa jumla. Baada ya kuangalia mengi ya kifani ambayo ni mwongozo wa sura zinazofuatia, tumezitamzama na kuzihakiki tungo za mwalimu Mbega katika misingi ya yaliyopitiwa katika sura za kwanza na pili. Maswala ya nadharia ya urasimu na mwongozo wake vimezingatiwa katika kuhakiki tungo hizo. Sura ya tatu inahusu uhakiki kifani wa upisho wa umalenga, huku sura ya nne ikishughulikia maswala ya kifani katika diwani ya Dafina ya Umalenga. Sura ya tano ni hitimisho ambapo kwa njia ya muhtasari imethibitisha haipothesia pamoja na kushughulikia maswala mengine ya kifani. Tasnifu hii ina sura tano zinazoshughulikia maswala ya kifani. Kwa sababu ambazo hatukuweza kuziepuka, alama za kufungia maneno zimetokea zikiangalia upande mmoja. Hii ni kwa sababu, ya aina ya kompiuta iliyotumiwa ambayo haina alama za kufungia. Tunaomba radhi kwa makosa hayo .en
dc.language.isoenen
dc.publisherUniversity of Nairobien
dc.titleFani katika ushairi wa Hassan Mwalimu Mbega: uhakiki wa upisho wa umalenga na dafina ya umalengaen
dc.typeThesisen
local.publisherDepartment of Artsen


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record