Ugatuzi wa utamaduni wa kikoloni katika tamthilia za Ngugi Wa Thiong'o
Date
2006-06Author
Ng'ang'a , Samuel Irungu
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Tahakiki nyingi za kazi za kifasihi za Kiswahili ambazo zimefanywa kuhusiana na
ukoloni na ukoloni rnambo-leo zimejikita katika nadharia ya U-Marx. Tahakiki za aina
hiyo hubakia kuangazia suala la uhusiano wa kiuchumi kama kitovu cha harakati za
ukoloni na ukoloni mambo-leo. Kwa namna hiyo mahusiano ya kitamaduni katika
miktadha hiyo hufumbiwa macho. Utafiti huu ulitiwa chachu na ukweli huo pamoja na
kwamba ukoloni wa kitamaduni ulitangulia ule wa kiuchumi. Ni kupitia kwanza
kuwatawala watu kitamaduni ambapo kuwaondoa kutoka kwa mfumo wao wa kiuchumi
(waliouzoea) hadi katika mfumo mpya wa kiuchumi (wa watawala) huwezekana.
Utafiti huu umezishughulikia tamthilia za Ngugi wa Thiong'o kwa kuzingatia ukweli
huo. Katika sura ya kwanza, masuala ya kimsingi kuhusiana na utafiti yameshughulikiwa.
Haya ni utangulizi, tatizo la utafiti, nadharia tete, madhumuni, msingi wa kinadharia,
upeo na mipaka, fasili za istilahi zilizotumiwa kwa muktadha wa utafiti huu na
yaliyoandikwa kuhusiana na somo hili.
Sura ya pili imeshughulikia masuala ya lugha, fasihi, utamaduni, ukoloni na ubaadaukoloni.
Upembuzi wa kina umefanywa katika kubainisha uhusiano uliopo kati ya dhana
hizo. Sura hii imeyaangazia masuala ya kimsingi kuhusiana na nadharia ya baada-ukoloni
vilevile.
Sura ya tatu na ya nne nazo zimeshughulikia uhakiki wa kazi husika. Sura ya tatu
imeshughulikia tamthilia za Mtawa Mweusi na Kesho Wakati Kama Huu huku sura ya
nne ikishughulikia tamthilia za Nitaolewa Nikipenda na Mzalendo Kimathi.
Mwishowe katika hitirnisho, mapengo, mapendekezo na masuala muhimu ya ubaadaukoloni
kuhusiana na tamthilia zinazoshughulikiwa yanayoibuka katika uhakiki
yameangaziwa.
Citation
Masters thesis University of Nairobi 1993Publisher
University of Nairobi Department of linguistics and African languages, university of Nairobi
Description
The information material is in Swahili language