Show simple item record

dc.contributor.authorNg'ang'a , Samuel Irungu
dc.date.accessioned2013-05-02T12:25:12Z
dc.date.available2013-05-02T12:25:12Z
dc.date.issued2006-06
dc.identifier.citationMasters thesis University of Nairobi 1993en
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/18405
dc.descriptionThe information material is in Swahili languageen
dc.description.abstractTahakiki nyingi za kazi za kifasihi za Kiswahili ambazo zimefanywa kuhusiana na ukoloni na ukoloni rnambo-leo zimejikita katika nadharia ya U-Marx. Tahakiki za aina hiyo hubakia kuangazia suala la uhusiano wa kiuchumi kama kitovu cha harakati za ukoloni na ukoloni mambo-leo. Kwa namna hiyo mahusiano ya kitamaduni katika miktadha hiyo hufumbiwa macho. Utafiti huu ulitiwa chachu na ukweli huo pamoja na kwamba ukoloni wa kitamaduni ulitangulia ule wa kiuchumi. Ni kupitia kwanza kuwatawala watu kitamaduni ambapo kuwaondoa kutoka kwa mfumo wao wa kiuchumi (waliouzoea) hadi katika mfumo mpya wa kiuchumi (wa watawala) huwezekana. Utafiti huu umezishughulikia tamthilia za Ngugi wa Thiong'o kwa kuzingatia ukweli huo. Katika sura ya kwanza, masuala ya kimsingi kuhusiana na utafiti yameshughulikiwa. Haya ni utangulizi, tatizo la utafiti, nadharia tete, madhumuni, msingi wa kinadharia, upeo na mipaka, fasili za istilahi zilizotumiwa kwa muktadha wa utafiti huu na yaliyoandikwa kuhusiana na somo hili. Sura ya pili imeshughulikia masuala ya lugha, fasihi, utamaduni, ukoloni na ubaadaukoloni. Upembuzi wa kina umefanywa katika kubainisha uhusiano uliopo kati ya dhana hizo. Sura hii imeyaangazia masuala ya kimsingi kuhusiana na nadharia ya baada-ukoloni vilevile. Sura ya tatu na ya nne nazo zimeshughulikia uhakiki wa kazi husika. Sura ya tatu imeshughulikia tamthilia za Mtawa Mweusi na Kesho Wakati Kama Huu huku sura ya nne ikishughulikia tamthilia za Nitaolewa Nikipenda na Mzalendo Kimathi. Mwishowe katika hitirnisho, mapengo, mapendekezo na masuala muhimu ya ubaadaukoloni kuhusiana na tamthilia zinazoshughulikiwa yanayoibuka katika uhakiki yameangaziwa.en
dc.language.isootheren
dc.publisherUniversity of Nairobien
dc.titleUgatuzi wa utamaduni wa kikoloni katika tamthilia za Ngugi Wa Thiong'oen
dc.typeThesisen
local.publisherDepartment of linguistics and African languages, university of Nairobien


Files in this item

FilesSizeFormatView

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record