Show simple item record

dc.contributor.authorKalota, Elizabeth
dc.date.accessioned2013-05-02T13:13:20Z
dc.date.available2013-05-02T13:13:20Z
dc.date.issued2006
dc.identifier.citationMaster of Artsen
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/18441
dc.description.abstractMadhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni kulishughulikia suala la udhalimu dhidi ya wahusika wa kike kama linavyojitokeza katika kazi za waandishi wa jinsia zote katika tamthilia za Kiswahili. Waandishi wa kike ni Penina Muhando, Hatia (1972) na Ari Katini Mwachofi, Mama ee (1987). Waandishi wa kiume nao ni A.S. Yahya na David Mulwa, Buriani (1983) na Said Ahmed Mohamed, Kitumbua Kimeingia Mchanga (2000). IIi kulifikia lengo letu, tulishughulikia tamthilia nne zilizoandikwa na waandishi wa kike na wa kiume na kuzichanganua. Pia tulipitia kazi mbalimbali zinazohusiana na mada ya utafiti iii kujifahamisha na masuala yanayohusu wanawake. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni kitengo kimoja cha ufeministi ambao ni ufeministi wa Kiafrika. Hii ni nadharia inayojaribu kueleza matatizo yanayowakabili wanawake wa Kiafrika, kinachoyasababisha najinsi wanavyoweza kujiepusha nayo. Matokeo ya utafiti huu yalionyesha kwamba, mwanamke anadhulumiwa na mifumo ya kiume katika taasisi ambazo zinajikita katika misingi ya ubabe - ume. Pia, yalibainisha kuwa udhalimu unaomkabili mwanamke una leta athari hasi kwa mwanamke na hata kwa jamii nzima. Mapendekezo ya utafiti huu yanaitaka jamii nzima kushirikiana iIi kumaliza udhalimu dhidi ya wanawake. Wanawake wanahimizwa kuwa katika mstari wa mbe\e iIi waweze kuutambua udhalimu dhidi yao na kupambana iIi kujikomboa. Utafiti wa baadaye kuhusu suala la udhalimu dhidi ya wahusika wa kike umependekezwa. Utafiti huo utachangia katika kulimulika suala hili kwa njia nyingine kwa lengo la kutafuta ukombozi kwa wahusika wa kike. Tasnifu hii imegawika katika faslu tano. Kila faslu imejadili kipengee maalum juu ya udhalimu dhidi ya wahusika wa kike. Kunatolewa hitimisho katika kila faslu ambapo msimamo na maoni ya tasnifu yanatolewa kwa mujibu wa yaliyojitokeza katika utafiti. Faslu ya kwanza ni utangulizi wa utafiti ambapo somo la utafiti, madhumuni ya utafiti, sababu za kuchagua mada, upeo na mipaka ya utafiti pamoja na nadharia tete zimeshughulikiwa. Aidha, msingi wa nadharia, yaliyoandikwa kuhusu somo hili pamoja na njia za utafiti zimeshughulikiwa. Faslu ya pili inashughulikia aina mbalimbali za udhalimu dhidi ya wahusika wa kike kama zinavyojitokeza katika kazi zilizoshughulikiwa pamoja na sababu zinazoleta udhalimu huo. Faslu ya tatu inabainisha athari za udhalimu dhidi ya wanawake. Athari ambazo zimejadiliwa ni pamoja na kusambaratika kwa ndoa, kuasi dini, woga, vifo na kukata tamaa. Katika faslu ya nne, mitazamo tofauti ya waandishi wa kazi zilizoshughulikiwa imeangaziwa iIi kuonyesha ulinganifu na tofauti zinazojitokeza kati ya waandishi wa jinsia zote. Faslu ya tano ni mahitimisho ambapo muhtasari wa matokeo ya utafiti, mapendekezo pamoja na tafiti za baadaye zimeshughulikiwa.en
dc.language.isootheren
dc.publisherUniversity of Nairobi.en
dc.titleUdhalimu dhidi ya wahusika wa kike katika tamthilia za kiswahilien
dc.typeThesisen
local.publisherDepartment of Kiswahilien


Files in this item

FilesSizeFormatView

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record