Uhakiki linganishi wa kifani wa tenzi za mikidadi na mavasa na swifa va nguvumali
Abstract
Tasnifu hii ni juu ya uhakiki-linganishi wa ki-fani wa tenzi za Swifa ya
Nguvumali (S Y N M) na Mikidadi na Mayasa(M N M). Utenzi wa M N M
ulitungwa na SaidAbdallah Masudiel Buhry miaka mingi kabla ya Karne ya
Ishirini. Utenzi huu umetafsiriwa kwa Kiingerezana J.W. Allen (1971) lakini
haujafanyiwa uhakiki wa aina yoyote. Unasimuliajuu ya mashujaa wawili
wa Kiislamu, Mikidadi na Mayasa na jinsi walivyoshinda pingamizi
walizowekewa na baba yake Mayasa ili wasioane. Utenzi wa SY N M
ulitungwa na Bwana Hasan bin Ismail (1968). Umehaririwa na
kutarjumiwa kwa Kiingereza na Peter Lienhardt (1968). Utenzi huu
umefanyiwa utafiti na Prof. M. H. Abdulaziz (1968), allyehakikl matumizi
ya lugha. Utafiti huo uliendelezwa na E. Kadenge Kazungu (1982)
aliyehakiki ukiushi wa kaida za lugha katika utenzi huu. Katika uchunguzi
wake, E. K. Kadenge amekipa kipengele cha tamathali za usemi nafasi
muhimu. Utafiti wetu umeenda mbali kwa kuvihakiki vipengele vyote vya
fani kama vile wahusika, mtindo, muundo, ploti, mandhari na
kuvilinganisha katika tenzi husika. raswa hivyo, tutalinganisha tenzi. hizi
mbili kifani kwa kuangalia jinsi fani yake inavyolingana au kutofautiana
kwa kuzingatia kuwa tenzi hizi zilitungwa kwa nyakati na mazingira
mbalimbali.
Mwongozowetu katika tasnltu hii ni nadharia ya Urasmi ambayo huangalia
fasihi kama sanaa ya maneno. Tumelinganisha fani na vipengele vyake
katika tenzi hizi mbili kwa kutambulisha kila mojawapo na kuchanganua
maana na uamilifu wake katika muktadha wa matumizi.
Kazi yetu imegawanywa katika sura nne. Sura ya kwanza ni utangulizi
unaoeleza somo la utafiti, madhumuni ya tasnifu, sababu za kuchagua
somo hili, madhumuni ya somo, upeo na mipaka, msingi wa nadharia,
nadharia tete na njia tulizotumia kufanyia utafiti huu. Katika sura hii pia
tumerejelea kazi mbalimbali zilizofanywa kuhusu somo hili.
Katika sura ya pili tumejadili dhana ya fani. Tumeshughulikia vipengele
vya fani kwa kurejelea wataalamu na wahakiki mbalimbali pamoja na
maoni yetu juu ya kunga hizo. Katika sura ya tatu tumelinganisha kila
mojawapo ya vipengele vya fani vinavyojitokeza katika tenzi za M N M
na S Y N M.
Sura ya nne ni hitimisho ambapo tumeelezea pale tulipofikia katika utafiti
wetu. Katika sura hii pia tumetathimini haipothesia ya utafiti wetu pamoja
na kuonyesha kama tumeweza kuifikia au la. Vilevile tumetoa
mapendekezo yetu.
Publisher
Idara va Isimu na lugha za kiafrika, Chuo kikuu cha Nairobi
Description
Shahada ya Uzamili (M. A.)