Show simple item record

dc.contributor.authorMungai, Paul K
dc.date.accessioned2013-05-02T13:44:31Z
dc.date.available2013-05-02T13:44:31Z
dc.date.issued2005-07
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/18463
dc.descriptionShahada ya Uzamili (M. A.)en
dc.description.abstractTasnifu hii ni juu ya uhakiki-linganishi wa ki-fani wa tenzi za Swifa ya Nguvumali (S Y N M) na Mikidadi na Mayasa(M N M). Utenzi wa M N M ulitungwa na SaidAbdallah Masudiel Buhry miaka mingi kabla ya Karne ya Ishirini. Utenzi huu umetafsiriwa kwa Kiingerezana J.W. Allen (1971) lakini haujafanyiwa uhakiki wa aina yoyote. Unasimuliajuu ya mashujaa wawili wa Kiislamu, Mikidadi na Mayasa na jinsi walivyoshinda pingamizi walizowekewa na baba yake Mayasa ili wasioane. Utenzi wa SY N M ulitungwa na Bwana Hasan bin Ismail (1968). Umehaririwa na kutarjumiwa kwa Kiingereza na Peter Lienhardt (1968). Utenzi huu umefanyiwa utafiti na Prof. M. H. Abdulaziz (1968), allyehakikl matumizi ya lugha. Utafiti huo uliendelezwa na E. Kadenge Kazungu (1982) aliyehakiki ukiushi wa kaida za lugha katika utenzi huu. Katika uchunguzi wake, E. K. Kadenge amekipa kipengele cha tamathali za usemi nafasi muhimu. Utafiti wetu umeenda mbali kwa kuvihakiki vipengele vyote vya fani kama vile wahusika, mtindo, muundo, ploti, mandhari na kuvilinganisha katika tenzi husika. raswa hivyo, tutalinganisha tenzi. hizi mbili kifani kwa kuangalia jinsi fani yake inavyolingana au kutofautiana kwa kuzingatia kuwa tenzi hizi zilitungwa kwa nyakati na mazingira mbalimbali. Mwongozowetu katika tasnltu hii ni nadharia ya Urasmi ambayo huangalia fasihi kama sanaa ya maneno. Tumelinganisha fani na vipengele vyake katika tenzi hizi mbili kwa kutambulisha kila mojawapo na kuchanganua maana na uamilifu wake katika muktadha wa matumizi. Kazi yetu imegawanywa katika sura nne. Sura ya kwanza ni utangulizi unaoeleza somo la utafiti, madhumuni ya tasnifu, sababu za kuchagua somo hili, madhumuni ya somo, upeo na mipaka, msingi wa nadharia, nadharia tete na njia tulizotumia kufanyia utafiti huu. Katika sura hii pia tumerejelea kazi mbalimbali zilizofanywa kuhusu somo hili. Katika sura ya pili tumejadili dhana ya fani. Tumeshughulikia vipengele vya fani kwa kurejelea wataalamu na wahakiki mbalimbali pamoja na maoni yetu juu ya kunga hizo. Katika sura ya tatu tumelinganisha kila mojawapo ya vipengele vya fani vinavyojitokeza katika tenzi za M N M na S Y N M. Sura ya nne ni hitimisho ambapo tumeelezea pale tulipofikia katika utafiti wetu. Katika sura hii pia tumetathimini haipothesia ya utafiti wetu pamoja na kuonyesha kama tumeweza kuifikia au la. Vilevile tumetoa mapendekezo yetu.en
dc.language.isoenen
dc.titleUhakiki linganishi wa kifani wa tenzi za mikidadi na mavasa na swifa va nguvumalien
dc.typeThesisen
local.publisherIdara va Isimu na lugha za kiafrika, Chuo kikuu cha Nairobien


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record