Uhakiki wa bina-damu! (2002) na Musaleo! (2004) na K.W. Wamitila.
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia suala la uhalisiajabu katika riwaya za fasihi ya Kiswahili. Riwaya
zilizohakikiwa ni Bina-Adamu!(2002) na Musaleo!(2004) za K.W. Wamitila. Nadharia
ilyoongoza utafiti huu ni kitengo kimoja cha mwelekeo wa usasaleo. Hii ni nadharia ya .
uhalisirjabu, matukio yanasawiriwa kiajabuajabu, ya kuogofya na kutisha. Matukio haya
huashiria hali halisi ya maisha katika jamii. Uhalisiajabu ni mtindo wa riwaya wa hivi majuzi
unaopiku njia za kimapokeo za uandishi wa fasihi ya Kiswahili na usawiri wa jamii.
Kimapokeo, riwaya inapaswa kujengeka katika misingi ya uhalisia.
Tasnifu hii inajumla ya sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti. Hapa ndipo
tumeshughulikia mada ya utafiti, malengo yake, sababu za kuchagua mada na yaliyoandikwa
kuhusu somo hili. Aidha, tumejadili upeo na mipaka ya utafiti huu na misingi ya nadharia
iliyotuongoza; rnwishowe tumeeleza mbinu za utafiti.
Sura ya pili imejadili maisha ya mwandishi, K. W. Wamitila. Tumeonyesha vipindi
mbalimbali vya uandishi wake. Uchunguzi huu umedhamiria kuonyesha mitindo aliyoitumia
tangu aanze kuandika na kuonyesha ni kwenye kipindi gani cha uandishialiingilia uandishi
wa kihalisiajabu na kwa nini alifanya hivyo.
Sura ya tatu na ya nne zinachunguza namna riwaya hizi mbili zimetumia uhalisiajabu katika
kuwasilisha ujumbe. Tumeonyesha mihimili ya nadharia ya uhalisiajabu aliyoitumia.
Mihimili hii ni pamoja na matukio ya kiajabuajabu, ndoto na uhalisia, uduara wa wakati,
visasili, uvunjaji wa mipaka ya mahali na upekee wa mtindo wa riwaya ya kihalisiajabu.
Sura ya tano imehakii na kulinganisha na kulinganua Eiwaya zote mbili kwa mujibu wa
mada husika. Aidha, matokeo ya utafiti, matatizo yaliyokabiliwa katika utafiti na
mapendekezo, yametolewa katika sura hii.
Citation
M.A (Swahili) 2005 ThesisSponsorhip
University of NairobiPublisher
Depatment of Linguistics, University of Nairobi
Description
Master of Arts Thesis