Show simple item record

dc.contributor.authorNyabunga, Vince A
dc.date.accessioned2013-05-02T13:54:25Z
dc.date.available2013-05-02T13:54:25Z
dc.date.issued2005
dc.identifier.citationM.A (Swahili) 2005 Thesisen
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/18470
dc.descriptionMaster of Arts Thesisen
dc.description.abstractUtafiti huu umeshughulikia suala la uhalisiajabu katika riwaya za fasihi ya Kiswahili. Riwaya zilizohakikiwa ni Bina-Adamu!(2002) na Musaleo!(2004) za K.W. Wamitila. Nadharia ilyoongoza utafiti huu ni kitengo kimoja cha mwelekeo wa usasaleo. Hii ni nadharia ya . uhalisirjabu, matukio yanasawiriwa kiajabuajabu, ya kuogofya na kutisha. Matukio haya huashiria hali halisi ya maisha katika jamii. Uhalisiajabu ni mtindo wa riwaya wa hivi majuzi unaopiku njia za kimapokeo za uandishi wa fasihi ya Kiswahili na usawiri wa jamii. Kimapokeo, riwaya inapaswa kujengeka katika misingi ya uhalisia. Tasnifu hii inajumla ya sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti. Hapa ndipo tumeshughulikia mada ya utafiti, malengo yake, sababu za kuchagua mada na yaliyoandikwa kuhusu somo hili. Aidha, tumejadili upeo na mipaka ya utafiti huu na misingi ya nadharia iliyotuongoza; rnwishowe tumeeleza mbinu za utafiti. Sura ya pili imejadili maisha ya mwandishi, K. W. Wamitila. Tumeonyesha vipindi mbalimbali vya uandishi wake. Uchunguzi huu umedhamiria kuonyesha mitindo aliyoitumia tangu aanze kuandika na kuonyesha ni kwenye kipindi gani cha uandishialiingilia uandishi wa kihalisiajabu na kwa nini alifanya hivyo. Sura ya tatu na ya nne zinachunguza namna riwaya hizi mbili zimetumia uhalisiajabu katika kuwasilisha ujumbe. Tumeonyesha mihimili ya nadharia ya uhalisiajabu aliyoitumia. Mihimili hii ni pamoja na matukio ya kiajabuajabu, ndoto na uhalisia, uduara wa wakati, visasili, uvunjaji wa mipaka ya mahali na upekee wa mtindo wa riwaya ya kihalisiajabu. Sura ya tano imehakii na kulinganisha na kulinganua Eiwaya zote mbili kwa mujibu wa mada husika. Aidha, matokeo ya utafiti, matatizo yaliyokabiliwa katika utafiti na mapendekezo, yametolewa katika sura hii.en
dc.description.sponsorshipUniversity of Nairobien
dc.language.isoenen
dc.titleUhakiki wa bina-damu! (2002) na Musaleo! (2004) na K.W. Wamitila.en
dc.typeThesisen
local.publisherDepatment of Linguistics, University of Nairobien


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record