Show simple item record

dc.contributor.authorOsoro, Mogere G
dc.date.accessioned2013-05-03T12:52:07Z
dc.date.available2013-05-03T12:52:07Z
dc.date.issued2003
dc.identifier.citationMaster of Artsen
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/18743
dc.description.abstractTasnifu hii imeshughulikia uhakiki wa Riwaya za Said Ahmed Mohamed katika misingi ya kifeministi Riwaya tulizozitumia kama sampuli katika uhakiki huu ni nne nazo ni Asali Chungu (1977) Utengano (1980), Kiza Katika Nuru (1988) na Tata za Asumini (1990). Tasnifu hii ina sura tano. Katika sura ya kwanza tumejadili, somo la utafiti, sababu za kulichagua na madhumuni. Maelezo kuhusu mipaka na upeo wa tasnifu pia yametolewa katika sura hii. Katika sura hii pia tumeyajadili yaliyoandikwa kuhusu mada na hatimaye tumeelcza matawi mbalimbali ya nadharia tuliyotumia. Sura ya pili inahusu maudhui ya Kifeministi katika riwaya za Asali Chungu na Utengano. Tumetoa muhtasari wa riwaya hizi mbili, maudhui ya kisiasa, kie1imu, kisheria, kiuchumi, malezi ya mtoto wa kike na pia mwanamke katika ndoa. Sura ya tatu ni kama inaendelea kuyachunguza maudhui ya kifeministi lakini kwa kurejelea riwaya za Kiza Katika Nuru na Tata za Asumini. Mambo tuliyotazama ni pamoja na mwanamke na utamaduni, mwanamke kielimu mwanamke kisiasa na pia mwanamke kiuchumi. Sura ya nne inashughulikia suala la usawiri wa wahusika wa kike katika riwaya za S.A Mohamed. Sura ya tano ni hitimisho. Turnerejelea yale yote yaliyojadiliwa katika sura zote. Pia tumetoa maoni yetu na mapendekezo kuhusu kufanywa kwa uiafuti zaidi.en
dc.language.isootheren
dc.publisherUniversity of Nairobien
dc.titleUhakiki wa riwaya za Ahmed Mohamed katika misingi va kifeministien
dc.typeThesisen
local.publisherFaculty of Arts kiswahilien


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record