Dhana ya maisha katika novela mbili za Euphrase Kezilahabi: Nagona na mzingile
View/ Open
Date
1999Author
Mungah, Charles I
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Tasnifu hii imechunguza suala la maisha kati ya maudhui mengine katika
novel a mbili za kezilahabi • Nagana na Mzingile. Tasnifu hii ina sura tano.
Katika sura ya kwanza tumebainisha tatizo la utafiti. Aidha tumebainisha
madhurnuni ya tasnifu, sababu za kuchagua mada hii pamoja na mipaka ya
kazi hii. Waaidha tumefanya udurusu wa yalioandikwa kuhusu mada hii.
Nadharia ambayo tumetumia ni ya kisosholojia ambayo baadhi ya kanuni
zake ru kusaili mazmgira kazi ya kifasihi ilimoibuka na mazrngira
alimoandikia msanii.
Sura ya pili imeonyesha juhudi mbalirnbali za binadamu maishani katika
kujaribu kuelezea ukweli na uhalisi wa maisha yake. Juhudi za mashujaa
vilevile na asasi mbalimbali zimejadiliwa Elimu ya mwanadarnu na mipak a
yake katika kuelezea maana ya maisha imezungumziwa.
inaweza kupatikana maishani mwa binadarnu Hatimaye sura hii imechunguza
na kujadili dhana ya ukweli kama ambavyo msanii huyu amelisawiri suala hili
katika Nagona na Mzingile.
Katika sura ya nne tumeonyesha vile ambavyo mwandishi ameathiriwa na
mazingira alimoandikia na kuyamithilisha na mazingira ya kipindi ambacho
udhanaishi uliweza kupata mwamko mpya huko Magharibi Aidha
umebainisha kuwa maisha ya msanii huyu na athari alizopata kutoka kwa
waandishi na watetezi wa udhanaishi yameathiri mtazamo wake wa maisha
vikubwa.
Hatimaye katika sura ya tano tumehitimisha kwa kutoa maoni yetu kwa
ujumla kuhusu kazi hizi pamoja na masuala muhimu ambayo tumeyajadili
katika sura za mwanzo. Aidha tumependekeza kazi hizi zifanyiwe uhakiki
zaidi hasa kwa upande wa fani
Citation
Master of ArtsPublisher
University of Nairobi Faculty of Arts Kiswahili