Uhakiki wa kifani katika utenzi wa siri li asirali na utenzi wa mwana Fatuma
Abstract
Kazi hii tumeibawibu katika sura nne. Katika sura ya kwanza tumeangazia tatizo
letu la utafiti, sababu za kulichagua somo hili, madhumuni yetu, na nadharia tete
zinazotuongoza. Vilevile katika sura hii tumeeleza yaliyoandikwa kuhusu somo hili,
upeo na mipaka ya utafiti wetu, mbinu tulizotumia kutafiti pamoja na msingi wa nadharia
ambayo tumetumia.
Katika sura ya pili, tumejadili misingi mbalimbali ya uhakiki wa kifani.
Tumeeleza maana zake na jinsi misingi yenyewe inavyotumika katika uhakiki wa kifani.
Katika sura ya tatu, tumezihakiki tenzi hizi mbili ; Utenzi wa Siri Li Asirali na
Utenzi wa Mwana Fatuma kwa kutumia misingi ya uhakiki wa kifani kama
tulivyoifafanua katika sura ya pili. Na katika sura ya nne, ambayo ndio ya mwisho,
tumetathmini matokeo ya utafiti wetu pamoja na kutoa mapendekezo ya utafiti zaidi.