Sauti ya mwanamke dhidi ya ubabedume katika tamtihlia tatu za Kiswahili
Abstract
Utafiti huu umechunguza sauti ya mwanamke dhidi ya ubabedume kupitia nguvu ya hoja
kama mojawapo ya silaha mwafaka katika kumkomboa mwanamke. Tamthilia ,
zilizoteuliwa kuhakikiwa katika kazi hii ni tatu ambazo ni za Njogu K. (Zilizala), Wa
Mberia K. (Natala) na Arege T. (Chamchela).
Sura ya kwanza ni msingi wa utafiti, madhumuni, sababu za kuchagua mada, upeo na
mipaka ya utafiti pamoja na nadharia tete zilizotumika.Pia imejumuisha msingi wa
nadharia, yaliyoandikwa kuhusiana na mada hii, zikiwemo njia za utafiti zilizotumika
katika kazi hii.
Sura ya pili imeshugulikia kwa ufupi chanzo cha harakati za wanawake kutaka
kujikomboa, pamoja na nafasi ya lugha katika kumkomboa mwanamke, sifa za drama
katika harakati hizi, sura mbalimbali za ubabedume na sababu za kutaka kuwadhibiti
wanawake.
Sura ya tatu inashughulika na sauti ya mwanamke kupitia nguvu za hoja mbalimbali na
ufaafu wake katika kuumbua na kudengua chukulizi mbalimbali hasi za ubabedume
zitumiwazo kuwakandamiza na kuwadunisha wanawake. Matumizi haya ya nguvu za
hoja yameshughulikiwa kwa kina na kuonyesha jinsi sauti ya mwanamke kupitia nguvu
ya hoja ilivyo na uwezo wa kurnkomboa mwanamke kutokana na chukulizi hasi za muda
mrefu za ubabedume ambazo zimewarenga baadhi ya wanawake.
Utafiti huu umechunguza sauti ya mwanamke dhidi ya ubabedume kupitia nguvu ya hoja
kama mojawapo ya silaha mwafaka katika kumkomboa mwanamke. Tamthilia
zilizoteuliwa kuhakikiwa katika kazi hii ni tatu ambazo ni za Njogu K. (Zilizala), Wa
Mberia K. (Natala) na Arege T. (Chamchelai.
Sura ya kwanza ni msingi wa utafiti, madhumuni, sababu za kuchagua mada, upeo na
mipaka ya utafiti pamoja na nadharia tete zilizotumika.Pia imejumuisha msingi wa
nadharia, yaliyoandikwa kuhusiana na mada hii, zikiwemo njia za utafiti zilizotumika
katika kazi hii.
Sura ya pili imeshugulikia kwa ufupi chanzo cha harakati za wanawake kutaka
kujikomboa, pamoja na nafasi ya lugha katika kumkomboa mwanamke, sifa za drama
katika harakati hizi, sura mbalimbali za ubabedume na sababu za kutaka kuwadhibiti
wanawake.
Sura ya tatu inashughulika na sauti ya mwanamke kupitia nguvu za hoja mbalimbali na
ufaafu wake katika kuumbua na kudengua chukulizi mbalimbali hasi za ubabedume
zitumiwazo kuwakandamiza na kuwadunisha wanawake. Matumizi haya ya nguvu za
hoja yameshughulikiwa kwa kina na kuonyesha jinsi sauti ya mwanamke kupitia nguvu
ya hoja ilivyo na uwezo wa kumkomboa mwanamke kutokana na chukulizi hasi za muda
mrefu za ubabedume ambazo zimewarenga baadhi ya wanawake.
Sura ya nne nayo imeshughulikia kwa kina matokeo mbalimbali ya sauti ya mwanamke
iliyo na nguvu ya hoja katika tamthilia zote tatu. Aidha sura hii imetathimini kufaulu kwa
mwanamke katika kutetea msimamo na imani zake licha ya vitisho.
Sura ya tano inatoa muhtasari wa matokeo ya utafiti pamoja na mapendekezo ya utafiti
wa baadaye.
Publisher
University of Nairobi, Department of Kiswahili