Uchanganuzi wa makosa ya kifonolojia yanayofanywa na wazungumzaji wa kikamba wanapojifunza Kiswahili sanifu
Abstract
Utafiti huu unanura kuchanganua makosa ya kifonolojia yanayofanywa na wazungumzaji wa kikamba kama lugha ya kwanza wanapojifunza Kiswahili sanifu kama lugha yao ya pili. 1Ii kufikia malengo, utafiti huu umetumia nadharia ya lugha - kati kama ilivyopendekezwa na Selinker (1972) hasa mifanyiko yake mitano ya kisaikolojia. Hivyo ilibidi tupange kazi hii kwa sura tano kama
ifuatayo. Sura ya kwanza imeshughulikia utangulizi, tatizo la utafiti, madhumuni ya utafiti, nadharia tete, sababu za kuchagua mada hii, upeo na mipaka ya utafiti, yaliyoandikwa kuhusu mada hii, msingi wa kinadharia na njia za utafiti. Katika sura ya pili, tumeshughulikia, uainishaji wa fonimu za Kiswahili sanifu pamoja na fonimu za Kikamba. Hapo ndipo tumebainisha sifa bainifu za fonirnu
mbalimbali pamoja na kuangazia.
Katika sura hii tumeturnia uanishaji wa sifa bainifu kwa mwelekeo wa Chomsky & Hale (1968). Katika sura ya tatu tumelinganisha miundo ya silabi katika lugha ya Kikarnba na lugha ya Kiswahili sanifu ikiwa kuzitofautisha na kuangazia mifano mbalimbali. Katika sura ya nne tumechanganua data. Katika kufanya hivyo tumezingatia mihimili minne ya nadharia ya lugha - kati kama ilivyopendekezwa na Selinker (1972) Katika sura ya tano tumetoa muhtasari wa kazi nzima, hitimisho na mapendekezo. Hapa ndipo tumebaini ni kwa kiwango kipi tulivyoafikia malengo yetu.
Publisher
University of Nairobi, Kenya