Show simple item record

dc.contributor.authorWanjugu, Veronicah W
dc.date.accessioned2012-11-13T12:33:32Z
dc.date.available2012-11-13T12:33:32Z
dc.date.issued2010
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/handle/123456789/4769
dc.description.abstractLengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza na kubainisha sababu na athari za ubadilishajimsimbo wa lugha za Kiswahili na Kiingereza wa data iliyokusanywa kwa kurekodiwa katika Shule ya Upili ya Akiba, Kangemi, kwa kutumia nadharia ya ukubalifu wa mawasiliano ya Howard Giles. Kutokana na nadharia tete zilizoongoza utafiti huu, mambo yafuatayo yalikadiriwa: kwanza, kuwa sababu zinazochangia ubadilishaji-msimbo shuleni Akiba zinatokana na hali ya kiutambuzi; pili, kuwa sababu za kiutambuzi za ubadilishaji-msimbo zinahusiana na zile za kijamii na kibinafsi na tatu ni kuwa kuna athari zinazotokana na ubadilishaji-msimbo wenyewe. Ilithibitika kuwa, sababu za kiutambuzi za ubadilishaji-msimbo zinahusiana na zile za kijamii na kibinafsi, na pia kwamba kuna athari zinazotokana na ubadilishaji msimbo. Hata hivyo kuhusu sababu za ubadilishaji-msimbo kutokana na hali ya kiutambuzi, ni jambo ambalo halikuthibitishwa kikamilifu kwa sababu tulipata kuwa sio hali yenyewe pekee inayosababisha ubadilishaji-msimbo. Tasnifu hii ina sura tano. Sura ya kwanza imeshughulikia kwa muhtasari kile kinachofanywa katika utafiti huu kwa kutoa mwelekeo jinsi utafiti wenyewe utakavyofanyika. Inajumuisha tatizo la utafiti, madhumuni, nadharia tete, sababu za kuchagua mada upeo na mipaka, yaliyoandikwa juu ya mada na nadharia, msingi wa nadharia unaojumuisha vijenzi na msingi wa nadharia, mbinu za utafiti zinazojumuisha ukusanyaji na uchanganuzi wa data na umuhimu wa utafiti. Sura ya pili imeshughulikia ubadilishaji-msimbo kwa ujumla. Imeangazia dhana yenyewe ya ubadilishajimsimbo, aina zake, dhana zinazokaribiana nao, na sababu na athari zake. Sura ya tatu na ya nne zimehusika na uchanganuzi wa data kwa kutumia vijenzi na msingi wa nadharia ya ukubalifu wa mawasiliano juu ya sababu mbalimbali za ubadilishaji-msimbo na athari zake. Sura ya tano ni hitimisho la utafiti huu pamoja na mapendekezo.en_US
dc.language.isoen_USen_US
dc.publisherUniversity of Nairobi, Kenyaen_US
dc.titleSababu na athari za ubadilishaji-msimbo Shuleni: Utafiti katika shule ya upili ya Akibaen_US
dc.title.alternativeThesis (MA)en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record