Uhakiki Wa Fani Katika Ngano Tano Za Kiswahili
View/ Open
Date
2013Author
Oyoyo, Jenipher O
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Tasnifu hii imeshughulikia fani katika ngano teule za Kiswahili kwa
kutumia nadharia ya umuundo. Tasnifu hii ina sura sita.
Katika sura ya kwanza, tumeangalia tatizo la utafiti, madhumuni ya utafiti,
sababu za kuchagua mada ya utafiti na kuorodhesha nadharia tete za utafiti
huu. Katika sura hii pia tumeshughulikia yaliyoandikwa kuhusu mada, upeo
wa utafiti, msingi wa kinadharia na njia za utafiti. Tulitumia mbinu ya
maktabani kukusanya data tuliyohitaji na kuichanganua.
Katika sura ya pili, tumetoa maelezo kuhusu fani na vipengele vyake kama;
msuko wahusika, usimulizi, muundo na tamathali za usemi.
Sura ya tatu, imeangazia tathmini ya msuko, wahusika na usimulizi katka
ngano tatu za kibunifu kutoka jamii ya Waswahili.
Katika sura ya nne, vile vile tumechanganua msuko, wahusika na mbinu ya
usimulizi zilizotumika katika ngano kutoka jamii ya Waswahili vile vile.
Sura ya tano, imeshughulikia matumizi ya lugha na tamathali mbalimbali za
usemi kama zinavyojitokeza katika ngano tulizochambua.
Sura ya sita imezungumzia hitimisho tathmini na mapendekezo ya utafiti
wa baadaye.
Citation
Oyoyo,Jenipher O.;2013.Uhakiki Wa Fani Katika Ngano Tano Za Kiswahili.Publisher
University of Nairobi College of Humanities and Social Sciences