Show simple item record

dc.contributor.authorKaringe, Joyce W
dc.date.accessioned2013-11-13T09:43:24Z
dc.date.available2013-11-13T09:43:24Z
dc.date.issued2013-11
dc.identifier.citationKaringe,Joyce W.;Novemba,2013.Usawiri Wa Ndoa Katika Riwaya Ya Unaitwa Nani?.en
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/58866
dc.description.abstractKatika tasnifu hii, tumechunguza usawiri wa asasi ya ndoa katika riwaya ya Unaitwa Nani? ya K. W. Wamitila (2008). Tunatumia nadharia ya sosholojia ya fasihi kuihakiki riwaya hii. Tasnifu yetu ina na sura tano. Katika sura ya kwanza tumeeleza tatizo letu la uchunguzi, madhumuni ya utafiti wetu pamoja na nadharia tete. Tumeeleza sababu za kuchagua somo hili na misingi ya nadharia ya sosholojia. Hatimaye, tunachunguza yaliyoandikwa kuhusu somo hili, nadharia ya sosholojia ya fasihi na muhtasari wa riwaya ya Unaitwa Nani? (2008). Tumeeleza njia ambazo tumetumia katika utafiti wetu na mwishowe, hitimisho. Katika sura ya pili tumefiti jinsi asasi ya ndoa imesawiriwa katika riwaya ya Unaitwa Nani? (2008) kwa kuchanganua ndoa zilizoko katika riwaya husika na kutathmini mchango wa kila mwanandoa mhusika katika kuiimarisha au kuizorotesha ndoa yake. Katika sura ya tatu tumezichanganua changamoto zinazoikabili asasi ya ndoa kama zilivyosawiriwa katika riwaya ya Unaitwa Nani?. Katika sura ya nne tumechunguza mikakati ambayo jamii ya riwaya ya Unaitwa Nani? inatumia kuikomboa asasi ya ndoa isisambaratike. Sura ya tano imekuwa hitimisho la utafiti wetu. Tumetathmini kufaulu au kutofaulu kwa utafiti wetu kwa kutathmini matokeo ya uchunguzi wetu, ama yanalingana au hayalingani na madhumuni ya utafiti. Tumeangalia iwapo nadharia tete zetu zimethibitishwa kuwa za kweli au la. Tumetoa mapendekezo ya utafiti wa baadaye.en
dc.language.isoenen
dc.publisherUniversity of Nairobien
dc.titleUsawiri Wa Ndoa Katika Riwaya Ya Unaitwa Nani?en
dc.typeThesisen
local.publisherCollege of Humanities and Social Sciencesen


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record