Uhakiki Wa Maudhui Teule Katika Utenzi Wa Nabii Isa
View/ Open
Date
2013Author
Owallah, Kennedy O
Type
ThesisLanguage
enMetadata
Show full item recordAbstract
Utafiti huu unahusu uchanganuzi wa maudhui teule katika Utenzi wa Nabii Isa. Huu ni utenzi
wa miaka ya (1970) lakini una uyakinifu katika jamii ya kisasa kimaudhui.
Kazi hii imegawika katika sura tano. Katika sura ya kwanza tumeshughulikia mambo ya
kiutangulizi ambayo yanahusu mada ya utafiti, tatizo la utafiti, madhumuni ya utafiti, sababu
za kuchagua mada hii, nadharia tete, upeo na mipaka, msingi wa kinadharia na njia za utafiti.
Katika sura ya pili, tumefafanua dhana ya maudhui na baadaye kuangalia baadhi ya mihimili
inayotumika kama nguzo dhabiti za maudhui. Mihimili hii ndiyo imeweka msingi wa kukuza
zaidi na kuendeleza sura ya tatu kwa kuonyesha msingi wa kukusanya na kuchanganua data
ya utafiti wetu.
Sura ya tatu inahusu uchangunuzi wa maudhui teule katika Utenzi wa Nabii Isa. Baada ya
kuyachanganua maudhui haya katika sura hii. Sura yetu ya nne imejadili jinsi ambavyo
maudhui haya yameibua athari katika utenzi wenyewe na vilevile uyakinifu wake katika jamii
ya kisasa.
Sura ya tano na ya mwisho ni ya hitimisho la utafiti wetu. Katika sura hii, tumetoa
mapendekezo ya utafiti wa kimaudhui zaidi katika Utenzi wa Nabii Isa.
Citation
shahada ya uzamili (m.a)Publisher
University of Nairobi IDARA YA ISIMU NA LUGHA.
Description
Tasnifu hii imetolewa ili kutosheleza baadhi ya mahitaji ya
shahada ya uzamili (m.a) katika chuo kikuu cha Nairobi.