Nafasi ya mwanamke: Jinsi inavyotetewa katika nyimbo za taarab za zanzibar

View/ Open
Date
2013-06Author
Yego, Elizabeth K
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Utafiti huu unahusu uchambuzi wa maudhui katika nyimbo za taarab za Kibiriti Upele na
Tupendane Wabaya Waulizane.Nyimbo hizi ziliimbwa na Mwanaidi Shaaban na Mzee Yusuf.
Kazi hii imegawanywa katika sura sita.Katika sura ya kwanza tumeangazia maswala muhimu ya
utafiti wetu.Tumeelezea swala la utafiti,madhumuni na nadharia tete zilizotuongoza.Aidha
sababu za utafiti zimeelezwa pamoja na upeo na mipaka.Msingi wa nadharia wa utafiti
umefafanuliwa na yaliyoandikwa kuhusu mada yalijadiliwa.Mwisho,mbinu za utafiti
zimebainishwa na uchanganuzi wa data umefanywa.
Katika sura ya pili tulitanguliza kwa kueleza maana ya fani ya wimbo pamoja na kuzitolea
maelezo ya aina mbalimbali za fani hii.Tumewarejelea wataalamu mbalimbali walioshughulikia
fani hii.
Sura ya tatu na nne zimebainisha maudhui kwa kina katika nyimbo za Kibiriti Upele na
Tupendane Wabaya Waulizane mtawalia.
Katika sura ya tano tumebainisha matumizi ya lugha katika kuwasilisha ujumbe wa waimbaji
kwa hadhira.Sura ya sita ni hitimisho.Matokeo ya uchunguzi yalielezwa na mapendekezo ya
uchunguzi zaidi yakatolewa.
Citation
Shahada Ya Uzamili Katika Chuo Kikuu Cha Nairobi Juni, 2013Publisher
Idara Ya Isimu Na Lugha