Show simple item record

dc.contributor.authorOdhiambo, George O
dc.date.accessioned2013-11-20T12:08:43Z
dc.date.available2013-11-20T12:08:43Z
dc.date.issued2013-10
dc.identifier.citationShahada Ya Uzamili Katika Chuo Kikuu Cha Nairobi.en
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/59613
dc.description.abstractTasnifu hii ililenga kutathmini athari za Sheng katika dini ya Kikristo. Kwa jumla tasnifu hii ina sura tano. Katika kila sura, tumeshughulikia maswala na vipengele maalum ambavyo vinaingiliana na kukamilishana. Katika sura ya kwanza tumeshughulikia usuli wa tasnifu hii. Tumetangulia kwa kutoa maana na chimbuko la lugha ya Sheng. Vile vile tumefafanua kwa upana tatizo la utafiti, swala la utafiti, nadharia tete, sababu za kuchagua mada husika, msingi wa kinadharia, upeo na mipaka ya utafiti, njia za utafiti pamoja na umuhimu wa utafiti huu katika nyanja ya elimu na utafiti. Katika sura ya pili tumejadili mbinu mbalimbali za uundaji wa maneno ya Sheng. Mbinu hizi za uundaji wa maneno tumezichanganua kwa kukita katika kiwango cha isimu cha mofologia. Katika michakato yetu ya kuzichanganua mbinu hizi za uundaji wa maneno katika Sheng, tumeweza kabaini kwamba mengi ya maneno ya Sheng huwa yamekopwa kutoka katika lugha zingine hususan Kiingereza, Kiswahili na Kikuyu. Maneno haya yaliyokopwa aidha hutoholewa ili yachukue sauti na muundo wa kimofologia wa leksimu za Sheng (kibantu). pamoja na ukopaji na utohozi, maneno ya Sheng pia yameundwa kwa mbinu zingine za uundaji wa maneno, kama vile uambatishaji, uambishaji, upolisemia, onomatopia, uhulutishaji, ubunifu, kaleki, ujenzi ghairi, akronimu, ukatizaji, ubadilishaji silabi na unyumbuzi kapa. Maneno ya Sheng ambayo kiasili hayatokani na ukopaji ni maneno buniwa pekee. Mifano ya maneno haya asilia ya Sheng ni pamoja na: Sheng Tafsiri Ndai = Gari Nganya = Daladala Ukedi = Ukimwi Uchiwa = Urembo Mbus = Msichana - 12 - Dingo = Mwizi Bonoko = Gushi Deng’a = Chuma Hii ndio mifano ya maneno ambayo kiasilia tuliweza kubaini kwamba ni leksimu za Sheng. Katika sura ya tatu tumeweza kubaini kwamba Sheng huzitumia lekisu hizo ilizojiundia kwa mbinu mbalimbali za kimofologia ili kujiundia vifahiwa . Baadaye wanajamii lugha hii ya Sheng huvitumia vifahiwa hivyo katika kujitungia sentensi. Sentensi hizo huwa za viwango mbalimbali vya kisintaksia na kisemantiki na ndizo ambazo hufanikisha mawasiliano miongoni mwa wanajamii lugha hii ya Sheng. Mifano ya vifahiwa hivyo vya Sheng tumevijadili kwa kuvitolea tafsiri ya Kiswahili sanifu. Sentensi ambazo huundwa kutokana na vifahiwa hivi huwa hazieleweki bayana na watu wasioielewa Sheng au wasiolengwa. Mojawapo ya watu hawa ni Wakristo wenye umri wa juu kama vile wazazi pamoja na vijana wasioilewa Sheng. Kundi hili la watu wasioielewa Shenge huitwa “fala,” jina ambalo huwa na lengo la kuwadunisha na kuwafedhehesha watu hawa. Kwa kiwango kikubwa, sentenzzi hizi za Sheng tumeweza kuzichanganua kwa vigezo vya kisintaksia ila kwa juujuu tu. Hii ilitokana na sababu kwamba tulilenga kukita katika semantiki wala sio katika sintaksia. Hata hivyo matawi haya mawili yote huingiliana na kukamilishana kwa ujumla na misingi ya isimu. Katika sura ya nne tumepata kufahamu kwamba wanajamii lugha ya Sheng huzitumia sentensi ilizojiundia kutokana na vifahiwa mbalimbali kwa kujieleza hasa kupitia sanaa ya uimbaji. Nyimbo ambazo tumeziangazia ni nyimbo za Kikristo wala sio za kidunia. Hii ilitokana na sababu kwamba utafiti wetu ulikita katika kutathmini athari za Sheng katika dini ya Kikristo. Hivyo tumepata kubaini kwamba Sheng ina athari zake katika asasi na taasisi mbalimbali za kijamii na kidini. Mifano ya taasisi na asasi hizi ni pamoja na makanisa (ya awali na ya kisasa nchini Kenya), na vyombo vya habari. Mifano ya makanisa ya awali tuliochanganua ni pamoja na kanisa la Katoliki, kanisa la SDA, kanisa la Angilikana, kanisa la PCEA, kanisa la A.C.K na kanisa la ‘Quackers. Mifano ya makanisa ya kisasa ambayo tumeangazia ni pamoja na “The Holy Ghost Fire Ministry”, “Jesus is Alive Ministry”, na “God’s Favour Ministry” - 13 - Kati ya aina hizi mbili za makanisa, tumepata kubaini kwamba makanisa ya kisasa ndiyo ambayo yamekubali matumizi ya Sheng kwa kiwango kikubwa katika kufanikisha taratibu za ibada. Athari za Sheng katika makanisa ya awali bado hazijaanza kuchipuza ingawaje dalili zipo. Taasisi nyngine ya kijamii ambayo tuliweza kubaini kwamba athari za Sheng hujithirihisha kwayo ni taasisi ya habari na mawasiliano. Mifano ya vyombo vya habari ambavyo tumeviangazia ni redio, televisheni na vijisahani vya santuri. Katika sura ya tano, tumeweza kujadili hitimisho la tasnifu hii. Vile vile tumeweza kujadili mambo ibuka ambayo hatukuwa tumeyajumuisha katika malengo na haipothesia zetu. Mambo haya ibuka ni pamoja na Sheng kutumiwa kwa kuyabuni makundi maovu ya watoto ambayo yana lengo la kuwafundisha na kuwahimiza watoto wasiwatii wazazi wao na watu wazima. Mfano wa kundi la aina hii ambalo tuliweza kulibaini ni kundi linalojulikana kama “Gaza”. Pia katika sura hii ya tano tumengazia maswala ya kijumla hususan yanayohusu matokeo ya utafiti wetu. Aidha tumependekeza baadhi ya maswala ambayo watafiti wa baadaye wataweza kuyaangazia kwa kina katika tafiti za baadaye.en
dc.language.isootheren
dc.publisherUniversity of Nairobien
dc.titleAthari za sheng katika dini ya Kikristo: Mtaa wa Umoja.en
dc.typeThesisen
local.publisherDepartment Of Linguistics And Languagesen


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record