Matumizi ya takriri na sitiari katika utenzi wa rasi’lghuli
View/ Open
Date
2013-10Author
Ndumbu, Justus M
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Utafiti huu unashughulikia matumizi ya takriri na sitiari katika Utenzi wa Rasi’lGhuli.
Tasnifu hii ina sura tano, katika sura ya kwanza tumetanguliza kuhusu mada
tuliyoshughulikia,usuli, tatizo la utafiti, malengo ya utafiti, nadharia tete, sababu za
kuchagua mada hii, upeo na mipaka, yalioandikiwa kuhusu mada hii, mbinu za utafiti na
msingi wa nadharia ya utafiti.
Katika sura ya pili tumejadili tamathali za usemi,dhana ya fani, takriri, aina za takriri
kama vile takriri irabu/vokali, takriri konsonanti, takriri neno/maneno na takriri silabi. Pia
tumerejelea ufafanuzi wa sitiari kama tamathali ya usemi, aina za sitiari kama vile sitiari
ya usuli, sitiari radidifu, sitiari ya kikaida, sitiari hisimseto na sitiari mseto.
Katika sura ya tatu tumeshughulikia kwa kina matumizi ya sitiari katika Utenzi wa
Rasi’lGhuli. Tumetoa mifano mahsusi ya aina za sitiari ambazo zilijitokeza kwa wingi.
Pia tumependekeza beti kadhaa ambazo mbinu hii ya sitiari imetumiwa katika utenzi
mzima.
Kama vile ilivyo sura ya tatu, katika sura ya nne tumejikita katika ufafanuzi wa takriri
katika kufanikisha kazi ya mtunzi kifani. Tumechunguza aina za takriri na jinsi
zilivyotumika katika Utenzi wa Rasi’lGhuli. Tumetoa mifano kadha wa kadha kutoka
kwa utenzi wenyewe na kupendekeza beti zaidi za kurejelewa.
Baadaye katika sura ya tano tumetathmini malengo ya utafiti pamoja na nadharia tete.
Kulingana na maoni yetu, tulifanikiwa kutimiza malengo yetu, pamoja na kuthibitisha
nadharia tete ambazo tulitoa mapendekezo ya yale ambayo yanahitajika kufanywa katika
Utenzi wa Rasi’lGhuli. Yakiwemo uchunguzi wa kina katika vipengele kama, maudhui,
dhamira, mandhari, toni, usimulizi na kadhalika. Pia tulipendekeza matumizi ya nadharia
zingine katika kuhakiki utenzi wenyewe.
Citation
Shahada Ya Uzamili (m.a) Katika Kiswahili,chuo Kikuu Cha Nairobi,2013Publisher
University of Nairobi, Idara Ya Isimu Na Lugha