Show simple item record

dc.contributor.authorNdumbu, Justus M
dc.date.accessioned2013-11-21T08:28:08Z
dc.date.available2013-11-21T08:28:08Z
dc.date.issued2013-10
dc.identifier.citationShahada Ya Uzamili (m.a) Katika Kiswahili,chuo Kikuu Cha Nairobi,2013en
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/59718
dc.description.abstractUtafiti huu unashughulikia matumizi ya takriri na sitiari katika Utenzi wa Rasi’lGhuli. Tasnifu hii ina sura tano, katika sura ya kwanza tumetanguliza kuhusu mada tuliyoshughulikia,usuli, tatizo la utafiti, malengo ya utafiti, nadharia tete, sababu za kuchagua mada hii, upeo na mipaka, yalioandikiwa kuhusu mada hii, mbinu za utafiti na msingi wa nadharia ya utafiti. Katika sura ya pili tumejadili tamathali za usemi,dhana ya fani, takriri, aina za takriri kama vile takriri irabu/vokali, takriri konsonanti, takriri neno/maneno na takriri silabi. Pia tumerejelea ufafanuzi wa sitiari kama tamathali ya usemi, aina za sitiari kama vile sitiari ya usuli, sitiari radidifu, sitiari ya kikaida, sitiari hisimseto na sitiari mseto. Katika sura ya tatu tumeshughulikia kwa kina matumizi ya sitiari katika Utenzi wa Rasi’lGhuli. Tumetoa mifano mahsusi ya aina za sitiari ambazo zilijitokeza kwa wingi. Pia tumependekeza beti kadhaa ambazo mbinu hii ya sitiari imetumiwa katika utenzi mzima. Kama vile ilivyo sura ya tatu, katika sura ya nne tumejikita katika ufafanuzi wa takriri katika kufanikisha kazi ya mtunzi kifani. Tumechunguza aina za takriri na jinsi zilivyotumika katika Utenzi wa Rasi’lGhuli. Tumetoa mifano kadha wa kadha kutoka kwa utenzi wenyewe na kupendekeza beti zaidi za kurejelewa. Baadaye katika sura ya tano tumetathmini malengo ya utafiti pamoja na nadharia tete. Kulingana na maoni yetu, tulifanikiwa kutimiza malengo yetu, pamoja na kuthibitisha nadharia tete ambazo tulitoa mapendekezo ya yale ambayo yanahitajika kufanywa katika Utenzi wa Rasi’lGhuli. Yakiwemo uchunguzi wa kina katika vipengele kama, maudhui, dhamira, mandhari, toni, usimulizi na kadhalika. Pia tulipendekeza matumizi ya nadharia zingine katika kuhakiki utenzi wenyewe.en
dc.language.isootheren
dc.publisherUniversity of Nairobi,en
dc.titleMatumizi ya takriri na sitiari katika utenzi wa rasi’lghulien
dc.typeThesisen
local.publisherIdara Ya Isimu Na Lughaen


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record