Nafasi na utambulisho wa mwanamke katika natala na kifo kisimani

View/ Open
Date
2013-10Author
Kipyegon, Keter E
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Madhumuni katika utafiti wetu yalikuwa ni; kwanza kuchunguza taswira chanya ambazo
mwandishi anaangazia kumhusu mwanamke katika Natala na Kifo Kisimani. Pia,
tulichunguza changamoto zinazokabili mwanamke katika harakati zake za kujikomboa.
Katika kufikia madhumuni yenyewe, tulihitajika kusoma kwa mapana, kuhakiki na
kuvichambua vitabu vinavyohusu nafasi ya mwanamke. Pia, tulihitajika kusoma vitabu
vinavyoangazia nadharia ya Ufeministi.
Katika utafiti wenyewe, tuliongozwa na nadharia ya Ufeminsiti wa Kiafrika. Kwa
ujumla, nadharia ya Ufeministi ni nadharia yenye malengo maalum. Hulenga kuangalia
na kujaribu kutatua matatizo yanayowakabili wanawake katika jamii ya ki-ubabe-dume.
Kutokana na utafiti wetu, ilibainika kuwa Kithaka wa Mberia amefaulu vilivyo
kumsawiri mwanamke katika jamii ya ki-ubabedume. Anaonyesha nafasi chukivu
anayopewa mwanamke katika jamii ya aina hii. Licha ya hayo, mwandishi anatoa
mchango wake muhimu katika kumjenga mwanamke kihadhi.
Tasnifu yenyewe ina sura tano: sura ya kwanza inaangazia somo la utafiti, sura yenyewe
lina utangulizi, tatizo la utafiti, madhumuni, nadharia tete, sababu za kuchagua mada,
upeo na mpaka ya utafiti, misingi ya nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada na njia za
utafiti.
Sura ya pili inaangazia nafasi na utambulisho wa mwanamke kama unavyodhihirika
katika Natala (1997). Sura yenyewe inadokeza nafasi dhalilishi na dunishi katika
sehemu ya kwanza, na nafasi chanya katika sehemu ya pili. Sehemu ya tatu ni hitimisho.
Sura ya tatu inahusu nafasi na utambulisho wa mwanamke kama unavyojitokeza katika
Kifo Kisimani (2001). Sehemu ya kwanza inaangazia nafasi dhalilishi na dunishi.
Sehemu ya pili ni nafasi chanya, sehemu ya tatu ni hitimisho.
Sura ya nne inaangazia changamoto zinazokabili harakati za kumkomboa mwanamke.
Changamoto zenyewe ni za aina aina, kama yanavyodhihirika katika tamthilia hizi.
Sura ya tano ina hitimisho ya tasnifu yenyewe. Katika sura yenyewe, kuna ithibati
kubainisha kutimia kwa madhumuni ya utafiti wenyewe.
Citation
Tasnifu Hii Imetolewa Ili Kutosheleza Baadhi Ya Mahitaji Ya Shahada Ya Uzamili Katika Chuo Kikuu Cha NairobiPublisher
University of Nairobi Department of Linguistics and Languages