Show simple item record

dc.contributor.authorKipyegon, Keter E
dc.date.accessioned2013-11-21T12:31:57Z
dc.date.available2013-11-21T12:31:57Z
dc.date.issued2013-10
dc.identifier.citationTasnifu Hii Imetolewa Ili Kutosheleza Baadhi Ya Mahitaji Ya Shahada Ya Uzamili Katika Chuo Kikuu Cha Nairobien
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/59779
dc.description.abstractMadhumuni katika utafiti wetu yalikuwa ni; kwanza kuchunguza taswira chanya ambazo mwandishi anaangazia kumhusu mwanamke katika Natala na Kifo Kisimani. Pia, tulichunguza changamoto zinazokabili mwanamke katika harakati zake za kujikomboa. Katika kufikia madhumuni yenyewe, tulihitajika kusoma kwa mapana, kuhakiki na kuvichambua vitabu vinavyohusu nafasi ya mwanamke. Pia, tulihitajika kusoma vitabu vinavyoangazia nadharia ya Ufeministi. Katika utafiti wenyewe, tuliongozwa na nadharia ya Ufeminsiti wa Kiafrika. Kwa ujumla, nadharia ya Ufeministi ni nadharia yenye malengo maalum. Hulenga kuangalia na kujaribu kutatua matatizo yanayowakabili wanawake katika jamii ya ki-ubabe-dume. Kutokana na utafiti wetu, ilibainika kuwa Kithaka wa Mberia amefaulu vilivyo kumsawiri mwanamke katika jamii ya ki-ubabedume. Anaonyesha nafasi chukivu anayopewa mwanamke katika jamii ya aina hii. Licha ya hayo, mwandishi anatoa mchango wake muhimu katika kumjenga mwanamke kihadhi. Tasnifu yenyewe ina sura tano: sura ya kwanza inaangazia somo la utafiti, sura yenyewe lina utangulizi, tatizo la utafiti, madhumuni, nadharia tete, sababu za kuchagua mada, upeo na mpaka ya utafiti, misingi ya nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada na njia za utafiti. Sura ya pili inaangazia nafasi na utambulisho wa mwanamke kama unavyodhihirika katika Natala (1997). Sura yenyewe inadokeza nafasi dhalilishi na dunishi katika sehemu ya kwanza, na nafasi chanya katika sehemu ya pili. Sehemu ya tatu ni hitimisho. Sura ya tatu inahusu nafasi na utambulisho wa mwanamke kama unavyojitokeza katika Kifo Kisimani (2001). Sehemu ya kwanza inaangazia nafasi dhalilishi na dunishi. Sehemu ya pili ni nafasi chanya, sehemu ya tatu ni hitimisho. Sura ya nne inaangazia changamoto zinazokabili harakati za kumkomboa mwanamke. Changamoto zenyewe ni za aina aina, kama yanavyodhihirika katika tamthilia hizi. Sura ya tano ina hitimisho ya tasnifu yenyewe. Katika sura yenyewe, kuna ithibati kubainisha kutimia kwa madhumuni ya utafiti wenyewe.en
dc.language.isootheren
dc.publisherUniversity of Nairobien
dc.titleNafasi na utambulisho wa mwanamke katika natala na kifo kisimanien
dc.typeThesisen
local.publisherDepartment of Linguistics and Languagesen


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record