Show simple item record

dc.contributor.authorKatutu, Ruth M
dc.date.accessioned2013-11-25T16:01:15Z
dc.date.available2013-11-25T16:01:15Z
dc.date.issued2013-11
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/60231
dc.description.abstractTasnifu hii imeshughulikia mtindo katika Mfuko Mtupu na Hadithi Nyingine. Katika sura ya kwanza, mambo muhimu yanayojadiliwa ni; Utangulizi, Tatizo la Utafiti, Madhumuni ya Utafiti, Nadharia Tete, Sababu za Kuchagua Mada, Upeo na Mipaka ya tasnifu, Msingi wa Nadharia ya Utafiti, Yaliyoandikwa kuhusu mada hii na mwisho ni njia tulizotumia kukamilisha utafiti huu. Katika sura ya pili, utafiti wetu umejikita katika kuchunguza matumizi ya msamiati katika Mfuko Mtupu na Hadithi Nyingine. Tumeshughulikia jinsi mwandishi ameteua msamiati wake ili kuwasilisha ujumbe anaodhamiria kufikisha kwa hadhira yake. Sura ya tatu inahusu uchanganuzi wa mtindo kwa misingi ya kisintaksia katika Mfuko Mtupu na Hadithi Nyingine. Tumechunguza ukiushi katika baadhi ya kategoria za maneno. Pia tumejadili ukiushi katika sentensi ndefu, fupi na nafasi ya uakifishaji katika sintaksia ya diwani yenyewe. Tumemalizia sura hii kwa kujadili ukiushi unaoibuka kwa kutozingatia muundo wa kiima kiarifa. Katika sura ya nne, tumechanganua ukiushi wa kisemantiki katika diwani ya kazi hii ya Said Mohamed . Tumechunguza tamathali za usemi kama tashbihi, sitiari, kinaya, tashhisi, tanakuzi, majazi, tasifida, maswali ya balagha na chuku. Pia tumechunguza mbinu nyingine za lugha kama takriri, usambamba wa visawe, tanakali za sauti, kuchanganya ndimi, jazanda, methali, barua na nyimbo. Sura ya tano tumehitimisha kwa kurejelea yale tuliyojadili katika sura za awali hasa kwa kuangaza madhumuni, nadharia tete na nadharia tuliyotumiwa kuhakiki kazi hii. Kadhalika tumeonyesha mchango wetu kutokana na yale ambayo tumeshugulikia katika utafiti huu. Hatimaye, tumetoa mapendekezo yetu kwa wapenzi wa lugha ya Kiswahili.en
dc.language.isoenen
dc.publisherUniversity of Nairobi,en
dc.titleMtindo katika diwani ya mfuko mtupu na hadithi nyingineen
dc.typeThesisen
local.publisherDepartment of Kiswahilien


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record