Matumizi ya usonde nafsi na usonde jamii: mtazamo wa uhusiano
Abstract
MUHTASARI
Utafiti huu umeshughulikia matumizi ya usonde nafsi na usonde jamii katika mawasiliano ya
walimu na wanafunzi wa Kiswahili. Tumetumia nadharia ya uhusiano kwa sababu ya sifa ya
usonde ya kutegemea muktadha kwenye ufasiri wa maneno yake. Vivyo hivyo tumechagua
kutafitia usonde nafsi na usonde jamii ili kutathmini wazo la Marmaridou (2000) kuwa kategoria
hizi mbili za usonde zina mtagusano kiasi cha kuchukuliwa kuwa ni kategoria moja.
Utafiti huu ulifanywa kwa kutumia utafiti stahilifu kimaelezo kwa kuwa data ambayo
ilikusanywa ilikuwa katika umbo la maneno tamkwa ya walimu na wanafunzi. Hatua
zilizotumiwa katika ukusanyaji ni pamoja na kusikiliza, kurekodi na kuandika. Data
ilichanganuliwa kwa kutumia utaratibu wa kusimba pronomino pamoja na hatua za uzulishaji
katika utaratibu wa ufahamu katika nadharia ya uhusiano.
Hatimaye utafiti huu umeshikilia kuwa, katika lugha ya Kiswahili kuna uhusiano kati ya usonde
nafsi na usonde jamii hasa katika baadhi ya matumizi ya usonde nafsi. Kwa hivyo haipaswi
kushikilia kuwa usonde nafsi na usonde jamii ni kategoria moja ya usonde.
Citation
Tasnifu hii imetolewa ili kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu cha NairobiPublisher
Idara Ya Kiswahili, University of Nairobi