Show simple item record

dc.contributor.authorMaina, Veronica
dc.date.accessioned2012-11-13T12:42:37Z
dc.date.available2012-11-13T12:42:37Z
dc.date.issued2005
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/handle/123456789/6283
dc.description(data migrated from the old repository)
dc.description.abstractTasnifu hii imeshughulikia nafasi ya mwanamke katika ushairi wa Shaaban Robert na imejikita katika tenzi zake mbili ambazo ni "Hati"na "Adili". Tasnifu hii ina sura nne. Kuna orodha ya vitabu vya marejeleo na kisha kiambatisho A-"Hati" na B - "Adili". Katika sura ya kwanza, tumeonyesha tatizo la utafiti. Aidha, tumeeleza kusudi la utafiti huu, sababu za kuchagua mada hii, upeo na mipaka ya utafiti, msingi wa kinadharia na njia za utafiti. Katika kazi hii, tumetumia tawi la nadharia ya ufeministi ambalo ni ufeministi as ilia ambalo linasisitiza uundaji wa jamii mpya ambayo itazingatia usawa wa wana kwa kuamini kuwa mabadiliko ya juujuu hayawezi kusaidia bali jamii izingatie mabadiliko ya miundo ya ndani ya kijamii. Sura ya pili inaelezea falsafa ya mshairi Shaaban Robert kuhusu maisha. Hapa tumeonyesha kuwa falsafa ya Shaaban imeathiriwa sana na dini, ukoloni na utamaduni kwa jumla. Katika sura hii, tumeanza kwa kuelezea maisha yake Shaaban. Aidha, tumeshughulikia mtazamo wake kuhusu maisha kwa kurejelea baadhi ya asasi mbalimbali za kitamaduni kama vile ndoa, dini, elimu n.k ambazo wanaufeministi wanadai kuwa huwa zinatumiwa na wanajamii ili kumdhulumu mwanamke. Katika sura ya tatu tumechunguza maudhui ya kifeministi lakini kwa kurejelea ushairi wa Shaaban tukiwa na lengo la kushughulikia nafasi ya mke katika "Hati"na "Adili". Kwa ufupi sura hii inashughulikia suala la nafasi ya mwanamke katika ushairi wa Shaaban hasa tukijikita katika "Hati"na "Adili". Sura ya nne ni hitimisho. Katika sura hii tumetoa maoni yetu kuhusu maswala tuliyoshughulikia katika tasnifu hii pamoja na mapendekezo ya kufanywa kwa utafiti zaidi.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Nairobi, CEES, Kenyaen_US
dc.subjectSwahili poetry -- Tanzaniaen_US
dc.subjectRobert, Shabanen_US
dc.titleNafasi ya mwanamke katika tenzi mbili za Shaban Robert : utenzi wa Hati na utenzi wa Adilien_US
dc.title.alternativeThesis (MA - Linguistics)en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

FilesSizeFormatView

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record