Muala na mshikamano katika Kiswahili: umuhimu wake katika uchangamuzi wa riwaya ya vipuli vya figo
Date
2005Author
Mulila, Asumpta Kamene-Matei
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Utafiti huu unahusu dhana za muala na mshikamano na jinsi zinavyochangia kujenga umatini katika riwaya ya Kiswahili.Malengo ya utafiti huu yalikuwa kuchunguza vipengele vinavyochangia kuleta muala na mshikamano katika Vipuli VyaFigo
Katika kulielezea suala la muala na mshikamano, mifano mbalimbali ya matini za lugha na fasihi ya Kiswahili imetolewa na kuchanganuliwa.
Uchunguzi wa vipengele vya muala na mshikamano katika riwaya ya Vipuli vya Figo umefanywa kwa kufuata mtazamo wa kinadharia wa muala (Halliday na Hasan 1976) na mtazamo wa kinadharia wa umatini (Beaugrande na Dressler 1981).
Sehemu mbalimbali za matini hii zimechukuliwa na kuchanganuliwa iIi kuonyesha mbinu za muala na mshikamano. Vijenzi vya kisanaa vya riwaya yenyewe; maudhui, ploti, hadithi, mandhari, wahusika na lugha vimejadiliwa kwa nia ya kuonyesha jinsi vinavyochangia uthabiti, ukubalifu na muumano wa riwaya hii.
Kutokana na uchunguzi uliofanywa, mahitimisho na mapendekezo yametolewa kufuatia matokeo ya uchunguzi wenyewe.Baadhi ya mapendekezo ni pamoja na kuchunguza muala na mshikamano katika aina nyingine za matini kama vile insha za wanafunzi na riwaya za kiusasaleo. Mchango mkubwa zaidi wa utafiti huu ni kuonyesha kwamba muktadha wa kiisimu pekee haujengi matini. Mahusiano ya kimuala pekee hayatoshi kuibainisha matini. Matini huwa matini kwa kutimiza kaida ambazo jamii-lugha ambamo imezalika huitarajia kutimiza. Muala (mahusiano ya kisarufi) ni mojawapo tu ya kaida hizi. Kwa hivyo, kwa maoni yetu, kipengele muhimu zaidi cha matini ni mshikamanol muumano. Mshikamano huu unatokana na hali ya matini kukubalika kama kipashio cha kisarufi, matini ya aina yake, na chombo cha mawasiliano cha jamii-Iugha yake.
Aidha,utafiti huu umeonyesha kwamba nadharia ya muala pekee haitoshi kupima umatini wa matini.Ipo haja ya kutumia nadharia kama vile ya umatini inayoweza kuchanganua vipengele vingine vya matini.Uchunguzi uliofanywa umebainisha kwamba urejelezi ndio aina ya muala unaopendelewa sana katika matini za kiusimulizi. Urejelezi nafsi hutumika zaidi ilhali urejelezi linganishi ni nadra katika matini za aina hii.
Publisher
University of Nairobi
Description
(data migrated from the old repository)