Show simple item record

dc.contributor.authorMulila, Asumpta Kamene-Matei
dc.date.accessioned2012-11-13T12:42:39Z
dc.date.available2012-11-13T12:42:39Z
dc.date.issued2005
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/handle/123456789/6292
dc.description(data migrated from the old repository)
dc.description.abstractUtafiti huu unahusu dhana za muala na mshikamano na jinsi zinavyochangia kujenga umatini katika riwaya ya Kiswahili.Malengo ya utafiti huu yalikuwa kuchunguza vipengele vinavyochangia kuleta muala na mshikamano katika Vipuli VyaFigo Katika kulielezea suala la muala na mshikamano, mifano mbalimbali ya matini za lugha na fasihi ya Kiswahili imetolewa na kuchanganuliwa. Uchunguzi wa vipengele vya muala na mshikamano katika riwaya ya Vipuli vya Figo umefanywa kwa kufuata mtazamo wa kinadharia wa muala (Halliday na Hasan 1976) na mtazamo wa kinadharia wa umatini (Beaugrande na Dressler 1981). Sehemu mbalimbali za matini hii zimechukuliwa na kuchanganuliwa iIi kuonyesha mbinu za muala na mshikamano. Vijenzi vya kisanaa vya riwaya yenyewe; maudhui, ploti, hadithi, mandhari, wahusika na lugha vimejadiliwa kwa nia ya kuonyesha jinsi vinavyochangia uthabiti, ukubalifu na muumano wa riwaya hii. Kutokana na uchunguzi uliofanywa, mahitimisho na mapendekezo yametolewa kufuatia matokeo ya uchunguzi wenyewe.Baadhi ya mapendekezo ni pamoja na kuchunguza muala na mshikamano katika aina nyingine za matini kama vile insha za wanafunzi na riwaya za kiusasaleo. Mchango mkubwa zaidi wa utafiti huu ni kuonyesha kwamba muktadha wa kiisimu pekee haujengi matini. Mahusiano ya kimuala pekee hayatoshi kuibainisha matini. Matini huwa matini kwa kutimiza kaida ambazo jamii-lugha ambamo imezalika huitarajia kutimiza. Muala (mahusiano ya kisarufi) ni mojawapo tu ya kaida hizi. Kwa hivyo, kwa maoni yetu, kipengele muhimu zaidi cha matini ni mshikamanol muumano. Mshikamano huu unatokana na hali ya matini kukubalika kama kipashio cha kisarufi, matini ya aina yake, na chombo cha mawasiliano cha jamii-Iugha yake. Aidha,utafiti huu umeonyesha kwamba nadharia ya muala pekee haitoshi kupima umatini wa matini.Ipo haja ya kutumia nadharia kama vile ya umatini inayoweza kuchanganua vipengele vingine vya matini.Uchunguzi uliofanywa umebainisha kwamba urejelezi ndio aina ya muala unaopendelewa sana katika matini za kiusimulizi. Urejelezi nafsi hutumika zaidi ilhali urejelezi linganishi ni nadra katika matini za aina hii.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.subjectSwahili literatureen_US
dc.subjectVipuli vya figoen_US
dc.titleMuala na mshikamano katika Kiswahili: umuhimu wake katika uchangamuzi wa riwaya ya vipuli vya figoen_US
dc.title.alternativeMasters Thesis (MA)en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

FilesSizeFormatView

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record