Show simple item record

dc.contributor.authorMoraa, Lydia
dc.date.accessioned2014-02-11T13:26:14Z
dc.date.available2014-02-11T13:26:14Z
dc.date.issued2013
dc.identifier.citationMoraa Lydia (2013). Matatizo Yanayodhihirika Katika Matini Tafsiri Za Kimatibabu: Utafiti Kielelezo Katika Hospitali Ya Kisii Level5en_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/64573
dc.description.abstractUtafiti wetu unahusu matatizo yanayodhihirika katika matini tafsiri za kimatibabu. Kwa kuwa taaluma ya kimatibabu ni pana, tuliteua sehemu nne za kurejelea katika utafiti huu. Sehemu hizi ni: magonjwa kwa jumla, dalili au ishara za magonjwa, tiba na uzuiaji. Tuliangazia matini zinazohusiana na sehemu tulizotaja kama zinavyodhihirika katika hospitali ya Kisii Level 5. Matatizo tunayorejelea ni ya kiisimu na yale yasiyokuwa ya kiisimu. Katika hospitali ya Kisii Level 5 kuna kikundi kiitwacho ‘Quality Improvement Team’ ambacho hujihusisha na kutafsiri matini hizi. Tafsiri hizi ni za kihuduma na ziko katika mabango, maagizo yaliyoandikwa, maelezo, vijikaratasi vya maelezo na vijitabu. Tafsiri za kimatibabu ni swala linalohitaji uangalifu mkubwa kwa kuwa huathiri afya ya mwanadamu. Kwa sababu ya kuchanganyika kwa watu kutoka jamii mbalimbali, tafsiri husaidia kupitisha ujumbe kutoka lugha moja hadi nyingine. Wadensjo (1998) anadai kuwa katika nchi nyingine, tafsiri zinazohusiana na sheria, afya na elimu zimeendelezwa kama taaluma za kiusomi (TY). Anaendelea kusema kuwa ni dhahiri kwamba wataalamu wa kimatibabu hawawezi kutoa huduma za kuridhisha za kiafya ikiwa hawawezi kuwasiliana vyema na wateja wao(uk 88, uk88). Hivyo basi tafsiri za kimatibabu ni jambo ambalo haliwezi kufanywa bila umakinifu unaohitajika. Gambier (2001) anadai kuwa tafsiri si kitendo rahisi cha kupitisha ujumbe kutoka lugha moja hadi nyingine ila ni kitendo changamano kinachohusu uakifishaji, njia za kueleza wakati, tarehe na mahali (TY). Maelezo haya ya Gambier yanawiana vyema na tunachosisitiza kuhusiana na tafsiri za kimatibabu. Vipengele alivyovitaja Gambier kama vile kuzingatia uakifishaji na wakati ni swala muhimu katika tafsiri za kimatibabu. Ushauri wanaotoa wahudumu wa kimatibabu huathiriwa na maelezo na wakati kwa mfano, tiba hasa kuhusu tembe huwa na maelezo ya wakati. Mtafsiri apitishe ujumbe usiokuwa na utata wa maagizo na maelezo katika karatasi za tembe. Badala ya kutaja kuwa tembe zitumike asubuhi, mchana na jioni, ni vyema kutaja wakati mahususi kama saa moja jioni kwa kuwa jioni huanza saa kumi.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.titleMatatizo yanayodhihirika katika matini tafsiri za kimatibabu: utafiti kielelezo katika Hospitali ya Kisii level 5en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record