Sajili ya maafisa wa polisi: tathmini ya matumizi ya lugha ya kiswahili katika kituo cha Polisi cha Central, Nairobi
Abstract
Utafiti huu ulilenga kubainisha sajili ya maafisa wa polisi kwa kujikita katika lugha ya
Kiswahili. Kazi yetu imepangiliwa katika sura tano ambapo sura ya kwanza tumeangazia
utangulizi, sura ya pili tumeshughulikia dhana tunazotumia katika utafiti, sura ya tatu
tumeonyesha na kubainisha data kwa mujibu wa nadharia yaBernstein ya misimbo na nadharia
ya Giles ya maafikiano ambapo tumeangazia mazungumzo baina ya maafisa wa polisi wenyewe.
Sura ya nne tumeonyesha na kuchanganua data kwa mujibu wa nadharia ya vitendo usemi kama
ilivyoelezwa na Austin na Searle kwa kujikita katika mazungumzo baina ya maafisa wa polisi na
wateja wao.
Mazungumzo baina ya maafisa wa polisi yamedhihirisha matumizi ya msimbo pana
wanapozungumzia mambo ya kijumla kama vile siasa na elimu na matumizi ya msimbo finyu
wanapozungumzia mambo ya usalama. Tumebainisha kuwa pana maafikiano baina ya maafisa
wa polisi kama kikundi cha kijamii kutokana na matumizi yao ya lugha. Mazungumzo baina ya
maafisa wa polisi na wateja wao yamedhihirisha kutokea kwa vitendo usemi ambavyo
vinadhihirisha athari ya sajili ya maafisa wa polisi. Usemi wa maafisa wa polisi umedhihirisha
vitendo usemi ambavyo huwa na sifa ya kutambulika kutokana na kinachosemwa na kani ya
ilokusheni. Ili kutaka kujua athari ya kitendo fulani, sharti kuangalia kinachosemwa, kinasemwa
wapi, na nani na kwa nani.
Publisher
University of Nairobi
Description
Thesis MA