Show simple item record

dc.contributor.authorBinyanya, Ruth M
dc.date.accessioned2014-11-25T12:24:41Z
dc.date.available2014-11-25T12:24:41Z
dc.date.issued2014
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/75312
dc.descriptionThesis MAen_US
dc.description.abstractUtafiti huu ulilenga kubainisha sajili ya maafisa wa polisi kwa kujikita katika lugha ya Kiswahili. Kazi yetu imepangiliwa katika sura tano ambapo sura ya kwanza tumeangazia utangulizi, sura ya pili tumeshughulikia dhana tunazotumia katika utafiti, sura ya tatu tumeonyesha na kubainisha data kwa mujibu wa nadharia yaBernstein ya misimbo na nadharia ya Giles ya maafikiano ambapo tumeangazia mazungumzo baina ya maafisa wa polisi wenyewe. Sura ya nne tumeonyesha na kuchanganua data kwa mujibu wa nadharia ya vitendo usemi kama ilivyoelezwa na Austin na Searle kwa kujikita katika mazungumzo baina ya maafisa wa polisi na wateja wao. Mazungumzo baina ya maafisa wa polisi yamedhihirisha matumizi ya msimbo pana wanapozungumzia mambo ya kijumla kama vile siasa na elimu na matumizi ya msimbo finyu wanapozungumzia mambo ya usalama. Tumebainisha kuwa pana maafikiano baina ya maafisa wa polisi kama kikundi cha kijamii kutokana na matumizi yao ya lugha. Mazungumzo baina ya maafisa wa polisi na wateja wao yamedhihirisha kutokea kwa vitendo usemi ambavyo vinadhihirisha athari ya sajili ya maafisa wa polisi. Usemi wa maafisa wa polisi umedhihirisha vitendo usemi ambavyo huwa na sifa ya kutambulika kutokana na kinachosemwa na kani ya ilokusheni. Ili kutaka kujua athari ya kitendo fulani, sharti kuangalia kinachosemwa, kinasemwa wapi, na nani na kwa nani.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.titleSajili ya maafisa wa polisi: tathmini ya matumizi ya lugha ya kiswahili katika kituo cha Polisi cha Central, Nairobien_US
dc.typeThesisen_US
dc.type.materialen_USen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record