Mikakati ya upole katika vipindi vya Runinga: Mawaidha na Bi.Msafwari katika Runinga ya Citizen
Abstract
Upole ni
suala
muhimu sana katika kuanzisha na
kudumisha mahusiano mema baina ya
wanajamii. Ili kudumisha mahusiano hayo, wazungu
mzaji wakati wote hulazimika kutumia
mikakati mbalimbali ya upole ili kuokoa nyuso zao na za
wenzao. Tasnifu hii ni uchunguzi wa
jinsi mikakati ya upole ilivyotumika katika vipindi vya runinga kwa kuangazia
vipindi vya
Mawaidha
na Bi.Msafwari
katika runinga ya
Citizen. Uchunguzi huu ulinuia kubainisha i
wapo
mazungumzo katika vipindi
hivi hujali ma
hitaji ya uso
ya wahusika,
pia
kujadili
mikakati ya
upole iliyotumika
katika vipindi hivi
na vilevile kubai
nisha iwapo nadharia ya uso ya Brown na
Levinson
(1978, 1987)
inaweza kutumiwa kufafanulia mikakati hiyo.
Ilibainika kuwa vipindi
vya Mawaidha na Bi. Msafwari hujali mahitaji ya uso na nadharia ya upole ya uso ni msingi
tosha wa kufafanulia mikakati husika ya upole. Kutokana
na matokeo ya uchunguzi huu,
tunapendekeza kuwa utafiti zaidi ufanywe kuhusiana na suala la upole katika vyombo
mbalimbali vya habari kwa kutumia nadharia tofauti na vipengele tofauti vya nadharia hizo.
Kwa
hakika upole ni dhana muhimu sana katika kila mazungumzo kwani umuhimu wa kuokoa nyuso
za wahusika hauwezi kusisitizwa
zaidi hasa katika mazungumzo k
wenye vipindi vya runinga
ambavyo kwavyo
maoni ya watazamaji pia hutiliwa maanani
Publisher
University of Nairobi
Description
Thesis