Show simple item record

dc.contributor.authorMulwa, Magdalene N
dc.date.accessioned2014-11-28T12:39:34Z
dc.date.available2014-11-28T12:39:34Z
dc.date.issued2014-11
dc.identifier.citationShahada ya uzamili katika idara ya Kiswahili ya chuo kikuu cha Nairobien_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/75643
dc.description.abstractUtafiti huu umechanganua taratibu za utohozi wa nomino za Kikamba kutoka Kiswahili kwa madhumuni ya kuainisha kanuni zinazohusika. Uchanganuzi umeongozwa na mtazamo wa Fonolojia ya vipande sauti huru ambao ni mojawapo ya mitazamo ya Fonolojia Zalishi. Kulingana na mtazamo huu, fonolojia ni mfumo sauti wenye rusu nne: rusu msingi, rusu fonimu, rusu silabi na rusu toni. Nadharia ya Mawimbi pia ilitumiwa kueleza sababu zilizochangia ukopaji katika lugha ya Kikamba. Utafiti wetu umeainisha nomino za Kikamba zilizokopwa kutoka Kiswahili, ukabainisha vigezo vya kifonolojia vilivyotumika na kuchanganua taratibu na kanuni za kifonolojia zilizofuatwa katika ukopaji huo. Vigezo vya fonolojia ya Kikamba ambavyo ni fonimu, silabi na sifa arudhi vimebainishwa. Pia, sababu zilizochangia ukopaji katika lugha ya Kikamba zimeelezwa. Data msingi ya utafiti ilikusanywa katika sehemu ya Kitui ya kati kupitia mbinu za mahojiano na uchunguzi wa kushiriki. Katika uwasilishaji, maelezo yameambatana na michoro na majedwali. Uchunguzi umedhihirisha kwamba katika kushughulikia maneno mkopo, mbinu tatu huhusika nazo ni: uchopekaji, udondoshaji na ugeuzaji maumbo. Utafiti wetu una nafasi ya kuchangia uwanja wa isimu lugha ya Kiafrika kwa jumla tukizingatia kwamba utohozi unaweza kutumika katika kulinganisha mifano ya fonolojia. Pamoja na haya, data ya matokeo ya uchunguzi wetu inaweza kuwasaidia wasomi wa isimu za lugha za Kiafrika. Vile vile, matokeo ya utafiti huu yanachangia kukua kwa lugha ya Kikamba kwani uchunguzi ulishughulikia mabadiliko yaliyofanyiwa maneno yaliyokopwa na hii ni njia moja ambayo lugha hutumia kukuza msamiati wakeen_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.titleFonolojia ya nomino-mkopo za kikamba kutoka Kiswahilien_US
dc.typeThesisen_US
dc.type.materialen_USen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record