Show simple item record

dc.contributor.authorWaweru, Teresia W
dc.date.accessioned2014-12-01T09:23:14Z
dc.date.available2014-12-01T09:23:14Z
dc.date.issued2014
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/75754
dc.description.abstractLengo kuu la utafiti huu lilikuwa kuangalia matumizi ya lugha katika Kanisa Katoliki kwa kuchanganua ubadilishaji msimbo katika mahubiri. Utafiti ulitumia data iliyokusanywa kwa kurekodiwa katika makanisa teule matatu kwa kutumia nadharia ya Umaanisho ya Grice (1975). Tuliongozwa na haipothesia zifuatazo; kwanza, kuwa ubadilishaji msimbo katika diskosi ya mahubiri unaathiri maana katika kiwango cha matumizi ya elementi za kiisimu. Pili, wahubiri katika Kanisa Katoliki hubadilisha msimbo. Tatu ubadilishaji msimbo katika diskosi ya mahubiri husababisha ukosefu wa urasmi na nne kiwango cha elimu, tabaka, tajriba, cheo na umri husababisha mabadiliko ya jinsi lugha inavyotumika. Ilithibitika kuwa ubadilishaji msimbo katika diskosi ya mahubiri unaathiri maana katika kiwango cha matumizi ya elementi za kiisimu, na kwamba wahubiri katika Kanisa Katoliki hubadilisha msimbo kwa wingi katika mahubiri ambapo ubadilishaji huu husababisha ukosefu wa urasmi. Aidha elimu, tabaka, tajriba, cheo na umri husababisha mabadiliko ya jinsi lugha inavyotumika. Tasnifu hii ina sura tano. Sura ya kwanza imeshughulikia kwa muhtasari kile kinachofanywa katika utafiti huu kwa kutoa mwelekeo jinsi utafiti wenyewe utakavyofanyika. Sura ya pili imeshughulikia ubadilishaji msimbo kwa kuzingatia mbinu na mikakati mbalimbali. Imeshughulikia pia msingi wa ubadilishaji msimbo na aina za ubadilishaji msimbo. Majukumu na athari za ubadilishaji msimbo pia zimezingatiwa. Baadaye ufungamano wa misingi ya ubadilishaji msimbo na Kanisa Katoliki umeshughulikiwa. Sura ya tatu na ya nne zimehusika na uchanganuzi wa data kwa kutumia vijenzi na msingi wa nadharia ya Umaanisho juu ya ubadilishaji msimbo wakati wa mahubiri katika Kanisa Katoliki. Sura ya tano ni hitimisho na muhtasari ambapo tumetoa maoni na mapendekezo.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.titleMatumizi Ya Lugha Katika Kanisa Katoliki: Uchanganuzi Wa Ubadilishaji Msimbo Katika Mahubirien_US
dc.typeThesisen_US
dc.type.materialen_USen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record