Fani Katika Nyimbo Teule Za Anastacia Mukabwa
Abstract
Utafiti huu ulishughulikia fani katika nyimbo za Anastacia Mukabwa kwenye albamu yake
kiatu kivue. Utafiti huu uliongozwa na msingi wa nadharia ya uhakiki wa kimtindo. Madhumuni
ya utafiti huu yalikuwa kuchunguza matumizi ya fani katika nyimbo za injili hasa kwa
kumrejelea mtunzi Anastacia Mukabwa.
Nyimbo ni mojawapo wa tanzu za fasihi simulizi ambazo zina mwelekeo wa matumizi ya lugha
yenye sauti zenye mahadhi na midundo zilizotengwa ili kunasa hisia za hadhira. Nyimbo
hunasibika kwa mpangilio maalum wa maneno, vipashio vya kiisimu, mada za kimaudhui,
kupitia midundo maalum na ujenzi wa taswira. Nyimbo huwakilisha mawazo, fikra na falsafa ya
mtunzi kwa njia inayosababisha changamoto na mawasiliano kwa hadhira lengwa. Kwa hivyo,
tuna ushahidi wa kutosha kwamba nyimbo za Kiswahili zina ukwasi mkubwa wa vipengele vya
kifani vinavyopaswa kuchunguzwa katika kiwango cha usomi. Utafiti huu ulishughulikia
matumizi ya fani kama kipengele cha kisanaa katika kazi ya fasihi, ni kipengele kinachojenga
umbo la kazi ya sanaa.
Utafiti huu ulidhihirisha kwamba nyimbo za Anastacia Mukabwa zina ukwasi mkubwa wa fani
kama vile wahusika, maudhui, mandhari, toni, tamadhali za semi, sitiari, ishara ,umbo na mtindo
Citation
Masters of KiswahiliPublisher
University of Nairobi