Show simple item record

dc.contributor.authorMburu, James M
dc.date.accessioned2014-12-01T09:39:29Z
dc.date.available2014-12-01T09:39:29Z
dc.date.issued2014
dc.identifier.citationMasters of Kiswahilien_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/75763
dc.description.abstractUtafiti huu ulishughulikia fani katika nyimbo za Anastacia Mukabwa kwenye albamu yake kiatu kivue. Utafiti huu uliongozwa na msingi wa nadharia ya uhakiki wa kimtindo. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kuchunguza matumizi ya fani katika nyimbo za injili hasa kwa kumrejelea mtunzi Anastacia Mukabwa. Nyimbo ni mojawapo wa tanzu za fasihi simulizi ambazo zina mwelekeo wa matumizi ya lugha yenye sauti zenye mahadhi na midundo zilizotengwa ili kunasa hisia za hadhira. Nyimbo hunasibika kwa mpangilio maalum wa maneno, vipashio vya kiisimu, mada za kimaudhui, kupitia midundo maalum na ujenzi wa taswira. Nyimbo huwakilisha mawazo, fikra na falsafa ya mtunzi kwa njia inayosababisha changamoto na mawasiliano kwa hadhira lengwa. Kwa hivyo, tuna ushahidi wa kutosha kwamba nyimbo za Kiswahili zina ukwasi mkubwa wa vipengele vya kifani vinavyopaswa kuchunguzwa katika kiwango cha usomi. Utafiti huu ulishughulikia matumizi ya fani kama kipengele cha kisanaa katika kazi ya fasihi, ni kipengele kinachojenga umbo la kazi ya sanaa. Utafiti huu ulidhihirisha kwamba nyimbo za Anastacia Mukabwa zina ukwasi mkubwa wa fani kama vile wahusika, maudhui, mandhari, toni, tamadhali za semi, sitiari, ishara ,umbo na mtindoen_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.titleFani Katika Nyimbo Teule Za Anastacia Mukabwaen_US
dc.typeThesisen_US
dc.type.materialen_USen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record