dc.description.abstract | Wanafunzi wanaojifunza lugha ya pili hufanya makosa mengi yakiwemo matamshi
mabaya ya maneno. Kutokana na hali hiyo, wanaisimu wamekuwa katika mstari wa
mbele kubaini chanzo cha makosa na vilevile kubuni mbinu faafu zinazochangia katika
kutatua matatizo hayo.
Utafiti huu ulinuia kutimiza malengo yafuatayo mathaalan; kuainisha makosa ya
kisintakisia katika kazi za wanafunzi kutoka kisiwani Mfangano, kuhakiki makosa
yanayojitokeza katika tungo za wanafunzi na pia kubaini kiwango cha makosa
yanayosababishwa na athari ya lugha ya kwanza. Kwa hivyo, kutokana na matokeo yetu,
tulibaini kuwa makosa mengi hujitokeza katika tungo za wanafunzi na pia ni wazi kuwa
makosa hujidhihirisha katika vipashio vyote vya lugha, ijapokuwa kwa asilimia tofauti
Nadharia iliyotumiwa katika kazi hii ni nadharia ya uchanganuzi linganuzi ambayo
huangazia ulinganuzi wa mifumo ya lugha mbili ili kubaini tofauti zinazojitokeza kati ya
lugha hizo. Kadhalika nadharia hii huchukulia kuwa makosa katika lugha ya pili
husababishwa na athari ya lugha ya kwanza.
Kwa muhstasari, kazi hii imemulika makosa ya kisintaksia ya wanafunzi kutoka kisiwani
Mfangano na aidha kubuni namna ya kukabiliana na makosa yanayosababishwa na lugha
ya kwanza. | en_US |