• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Uchanganuzi wa mchezo wa papa shirandula kimaudhui nakimtindo

    Thumbnail
    View/Open
    Full Text (637.0Kb)
    Date
    2014
    Author
    Waweru, Scholastica W
    Type
    Thesis; en_US
    Language
    en
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Tasnifu hii ni juu ya uchanganuzi kimaudhui na kimtindo wa mchezo wa‘Papa Shirandula’ unaoonyeshwa katika runinga ya ‘Citizen’. Mchezo huu umetungwa na Charles Bukeko na ulipeperushwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 2007 lakini haujafanyiwa uchanganuzi wa aina yoyote kimaudhui na kimtindo. Mchezo huu unasimulia maisha ya Papa Shirandula ambaye pia huitwa Wilberforce anayefanya kazi ya bawabu katika kampuni ya Anderson Holdings Company Limited. Papa Shirandula ni mhusika matata anayeunda mbinu nyingi ili kujikimu kimaisha na mara nyingi hutumia uwongo na hila ili afaidike si ajabu kwa majirani zake na mkewe Wilbroda yeye ni “meneja mkurugenzi” ilhali kwa hadhira ni bawabu. Utafiti huu umefungua ukurasa wa uchambuzi wa mchezo huu kwa kushughulikia maudhui na mtindo. Tumeshughulikia maudhui na vipengele vyake kama vile dhamira, falsafa, maadili na ujumbe. Katika mtindo tumejadili vipengele vya ploti, muundo, mandhari, wahusika na toni. Mwongozo wetu katika tasnifu hii ni nadharia ya umuundo ambayo huangalia jinsi kipindi hiki kilivyosukika kimaudhui na kimtindo ili kutimiza malengo yake. Pia, katika kazi hii tumeonyesha matokeo ya utafiti wetu na kisha kutoa mapendekezo tuliyoona yanafaa. Kazi hii imegawanywa katika sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi unaoeleza mada ya utafiti, madhumuni ya tasnifu, sababu za kuchagua mada hii, upeo na mipaka, msingi wa nadharia, nadharia tete na njia tulizotumia kufanyia utafiti huu. Pia katika sura hii tumerejelea kazi mbalimbali zilizofanywa kuhusu mada hii.
    URI
    http://hdl.handle.net/11295/77053
    Citation
    Shahada Ya Uzamili
    Publisher
    University of Nairobi
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24385]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback