Mamlaka Na Itikadi Katika Nyimbo Teule Za Taarab
View/ Open
Date
2015Author
Makhulo, O Evans
Type
ThesisLanguage
othersMetadata
Show full item recordAbstract
Utafiti huu ulihusu uchunguzi wa mamlaka na itikadi katika nyimbo za taarab za Zilipendwa
ulioimbwa na Khadija Yusuf na Utalijua Jiji ulioimbwa na Afua Suleimani. Hili liliwezeshwa na
kuwepo kwa malengo matatu.Kwanza, kuchunguza utunzi na maudhui tawala katika nyimbo hizi
ili kubaini mafungamano ya masuala hayo na itikadi inayotawala.Pili,kuonyesha udhihirikaji wa
mahusiano ya mamlaka katika nyimbo hizo na mwisho, kueleza mikakati ya kipragamatiki na
mchango wake katika ujenzi wa mamlaka na itikadi katika hizo nyimbo.Sampuli lengwa
ilitumika kuziteua nyimbo hizi mbili na matini zake zikaandikwa baada ya kanda za nyimbo hizo
kusikilizwa.Baada ya kuandikwa, vishazi vyake vilichambuliwa kwa kutumia nadharia ya
Diskosi Changanuzi Tunduizi (DCT) na mtazamamo wa Isimu Amilifu wa Kimfumo (IAK).
Kutokana na uchambuzi huo, iligunduliwa kuwa itikadi ya ubabedume ndiyo inayotawala katika
nyimbo hizo na kwamba mahusiano ya mamlaka hujidhihirisha vilevile katika nyimbo
hizi.Muhimu zaidi ni kuwa maswala haya ya mamlaka na itikadi yanaweza kuonyeshwa kwa
kueleza mikakati ya kipragamatiki katika nyimbo hizo.Utafiti huu utakuwa muhimu kuhusu
namna ya kutumia vipengele vya kiisimu kuchanganua matini za lugha ya Kiswahili.
Publisher
University of Nairobi
Description
Thesis