Show simple item record

dc.contributor.authorMakhulo, O Evans
dc.date.accessioned2015-12-11T12:46:05Z
dc.date.available2015-12-11T12:46:05Z
dc.date.issued2015
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/93442
dc.descriptionThesisen_US
dc.description.abstractUtafiti huu ulihusu uchunguzi wa mamlaka na itikadi katika nyimbo za taarab za Zilipendwa ulioimbwa na Khadija Yusuf na Utalijua Jiji ulioimbwa na Afua Suleimani. Hili liliwezeshwa na kuwepo kwa malengo matatu.Kwanza, kuchunguza utunzi na maudhui tawala katika nyimbo hizi ili kubaini mafungamano ya masuala hayo na itikadi inayotawala.Pili,kuonyesha udhihirikaji wa mahusiano ya mamlaka katika nyimbo hizo na mwisho, kueleza mikakati ya kipragamatiki na mchango wake katika ujenzi wa mamlaka na itikadi katika hizo nyimbo.Sampuli lengwa ilitumika kuziteua nyimbo hizi mbili na matini zake zikaandikwa baada ya kanda za nyimbo hizo kusikilizwa.Baada ya kuandikwa, vishazi vyake vilichambuliwa kwa kutumia nadharia ya Diskosi Changanuzi Tunduizi (DCT) na mtazamamo wa Isimu Amilifu wa Kimfumo (IAK). Kutokana na uchambuzi huo, iligunduliwa kuwa itikadi ya ubabedume ndiyo inayotawala katika nyimbo hizo na kwamba mahusiano ya mamlaka hujidhihirisha vilevile katika nyimbo hizi.Muhimu zaidi ni kuwa maswala haya ya mamlaka na itikadi yanaweza kuonyeshwa kwa kueleza mikakati ya kipragamatiki katika nyimbo hizo.Utafiti huu utakuwa muhimu kuhusu namna ya kutumia vipengele vya kiisimu kuchanganua matini za lugha ya Kiswahili.en_US
dc.language.isoothersen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.titleMamlaka Na Itikadi Katika Nyimbo Teule Za Taaraben_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record