Matatizo Ya Mwanamke Katika Kidagaa Kimemwozea Na Nyuso Za Mwanamke
View/ Open
Date
2015Author
Ruto, Monica C
Type
ThesisLanguage
othersMetadata
Show full item recordAbstract
Kazi hii inashughulikia matatizo yanayomkabili mwanamke katika Nyuso za
Mwanamke (2010) ya Said A Mohammed na Kidagaa Kimemwozea (2012) ya
Ken Walibora na athari zake kwa jamii .Tuliangalia matatizo ya wanawake na
athari zinazotokana na matatizo hayo.
Pia tumeangazia mitazamo ya waandishi kuhusu udhalimu dhidi ya wahusika
wa kike . Sababu za kuchagua mada pia zimeelezwa. Yaliyoandikwa kuhusu mada
hii ni mengi kama tutakavyoona hapo baadaye.
Misingi ya Nadharia ya Ufeministi na mihimili yake ndiyo iliyoongoza utafiti
wetu. Nadharia hii ya Ufeministi ni kwa mujibu wa wahakiki kama Birke
(1986), Luvenduski, Randall (1993 ) na wengineo.
Nadharia ya Ufeministi inatumia fasihi kama jukwaa la kuelezea kwa uyakinifu
hali aliyomo mwanamke ili kumsaidia mtu yeyote kuielewa hali hiyo kama
mojawapo wa mihimili yake muhimu . Mbinu ya kusoma maktabani ilitumika,
ambapo tulirejelea makala mbalimbali yakiwemo majarida, tasnifu na vitabu
kwa lengo la kupambanua suala la utafiti na nadharia kwa kina.
Publisher
University of Nairobi