Show simple item record

dc.contributor.authorNyamemba, Rose
dc.date.accessioned2015-12-18T07:01:18Z
dc.date.available2015-12-18T07:01:18Z
dc.date.issued2015
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/93808
dc.description.abstractKatika tasnifu hii tumeonyesha maswala ya vijana na jinsi yanavyoshughulikiwa na waandishi katika diwani ya Tunu ya Ushairi ambayo ina mkusanyiko wa mashairi ya waandishi wanne tofauti.Waandishi hawa ni pamoja na Andanenga, Nyanje, Kiponda na Arege (2013). Utafiti huu umeonyesha kwamba vijana wana changamoto nyingi katika jamii ambazo ni lazima hatua ya dharura ichukuliwe ili kuokoa kizazi kijacho. Tumeshughulikia mashairi kumi na saba ambayo tulichagua kwa kutumia sampuli lengwa. Katika utafiti huu, nadharia ya uhalisia imetumika kuonyesha ukweli wa mambo katika jamii. Ukweli huu ni ule ambao unaweza kuonekana na kuthibitishwa pasi na tashwishi yoyote ile. Nadharia hii ya uhalisia iliwezesha kuhakiki maswala ya vijana katika jamii na jinsi waandishi wa diwani ya Tunu ya ushairi wanavyoshughulikia maswala hayo. Maswala haya ni pamoja na elimu, ukosefu wa maadili, umaskini, magonjwa, ukosefu wa malezi bora na ukosefu wa ajira. Baada ya kufanya utafiti wetu kwa kina tuligundua kwamba ni kweli vijana katika jamii tofauti huwa na changamoto sawa. Pia makisio yetu kuwa waandishi wote katika diwani ya Tunu ya ushairi wana mwelekeo sawa kuhusu vijana ni kweli kwa sababu maswala wanayoyashughulikia ni maswala ibuka katika jamii na yanawahusu vijana.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.titleUchanganuzi Linganishi Wa Maswala Ya Vijana Na Jinsi Yanavyoshughulikiwa Na Waandishi Katika Diwani Ya Tunu Ya Ushairien_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record