• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Uchambuzi Wa Mikakati Ya Upole Kama Inavyotumiwa Na Wahusika Wakuu Katika Tamthilia Ya Mbaya Wetu

    Thumbnail
    View/Open
    Full Text (633.8Kb)
    Date
    2015
    Author
    Machira, Stephen
    Type
    Thesis
    Language
    en
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Utafiti huu umeshughulikia suala la upole kama linavyobainika katika matumizi ya lugha ya wahusika wakuu katika tamthilia ya Mbaya Wetu. Mtafiti ametumia mtazamo wa Nadharia ya Upole ya Brown na Levinson (1987) na kujikita katika kipengele cha mikakati ya upole. Data ya uchunguzi huu ilitokana na uchambuzi wa kauli na matamshi ya wahusika wakuu katika tamthilia ya Mbaya Wetu. Lengo la kwanza la utafiti lilikuwa kubainisha iwapo wahusika wakuu katika tamthilia ya Mbaya Wetu wanaitumia mikakati ya upole katika kuokoa uso wanapoingiliana. Matokeo yanadhihirisha kuwa, wahusika wakuu katika tamthilia ya Mbaya Wetu wanaitumia mikakati ya upole wanapoingiliana kama njia ya kuyafanikisha mazungumzo yao. Lengo la pili la uchunguzi huu lilikuwa kubainisha jinsi sifa za wahusika wakuu katika tamthilia ya Mbaya Wetu zinavyobainika kupitia matumizi yao ya mikakati ya upole. Utafiti huu unaonyesha kuwa, sifa mbalimbali za wahusika wakuu zikiwemo hasi na chanya zinabainika kupitia matumzi yao ya mikakati ya upole.Vilevile, uchunguzi huu ulidhamiria kuzichunguza hali zinazoyaathiri matumizi ya mikakati ya upole inayotumiwa na wahusika wakuu katika tamthilia ya Mbaya Wetu. Matokeo yanaonyesha kuwa, matumizi ya mikakati ya upole na wahusika wakuu katika tamthilia ya Mbaya Wetu yanaathiriwa na hali mbalimbali za kijamii kama vile mamlaka na malengo yao. Kwa jumla, utafiti huu umebainisha kuwa, upole una nafasi kubwa katika kuikamilisha kazi nzima ya tamthilia. Kupitia uchunguzi huu, imethibitika kuwa, kufanikiwa kwa maingiliano ya wahusika katika tamthilia kunategemea kiwango chao cha matumizi ya mikakati ya upole.
    URI
    http://hdl.handle.net/11295/94529
    Publisher
    University of Nairobi
    Subject
    Tamthilia ya mbaya wetu
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24385]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback