Uhakiki Linganishi Wa Sifa Za Mashujaa: Sakawa Na Fumo Liyongo
View/ Open
Date
2015Author
Kemunto, Judith
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Kuna tafiti kadhaa zilizowahi kufanywa kuhusu majagina wa Kiafirika. Hata hivyo hakuna utafiti linganishi uliowahi kufanywa kuwahusu Fumo Liyongo na Sakawa. Tasnifu hii inazilinganisha sifa zao jinsi zinavyojitokeza katika Utenzi wa Fumo Liyongo (Kijumwa 1973) na Kivuli cha Sakawa (Matundura 2010) kwa kuzingatia nadharia ya uhakiki wa vikale. Historia yao pamoja na ya jamii wanamotoka mashujaa hawa zimechunguzwa ili kuweka msingi thabiti wa kuzichunguza sifa zao. Inadhihirika kwamba vikale hujitokeza katika vipindi na maeneo mbalimbali kwa kurejelea wakati na mazingira ambamo tungo hizi ziliandikwa. Isitoshe, vikale huwa havifungamanishwi na utanzu mmoja inavyobainika kutoka kazi hizi tulizozitumia katika utafiti huu. Kwa kuongozwa na ubia wa sifa za majagina utafiti umebainisha kwamba mashujaa hawa wana sifa kadha ambazo zinafanana kuliko zile zinazowatofautisha. Sifa zilizozingatiwa katika kuwalinganisha ni zile za kihistoria, kijamii na za kimaumbile
Publisher
University of Nairobi